Home Dauda TV Yanga ilibebwa, Stand United yalalamikia waamuzi

Yanga ilibebwa, Stand United yalalamikia waamuzi

10444
0
SHARE

Kocha msaidizi wa Stand United Athumani Bilali ‘Billo’ amewashushia lawama waamuzi waliochezesha mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Stand United kutokana na makosa yao kuigharimu timu yake na kupelekea kupoteza mchezo.

Billo amelalamikia kitendo cha line one kuinua juu kibendara wakati goli la kwanza linafungwa lakini badae akakishusha na mwamuzi wa kati akaashiria goli hilo ni halali mpira upelekwe kati.

“Tumepoteza mchezo kwa nguvu za waamuzi kwa sababu waliisaidia timu pinzani kwa makosa madogomadogo ya hapa na pale, goli la kwanza wakati linafungwa line one ananyoosha kibendera wachezaji wangu wakasimama Yanga wakafunga.”

“Waamuzi waliochezesha mchezo wetu dhidi ya Yanga mimi binafsi sijawafurahia.”

Kuhusu safu yake ya ushambuliaji kupoteza nafasi nyingi za kufunga magoli, Billo amesema ni kukukosa umakini lakini tatizo hilo litashughulikiwa na benchi la ufundi.

“Ni umakini mdogo wa washambuliaji wetu kwa sababu tumetengeneza nafasi saba tumefunga moja kwa hiyo hilo suala tutalifanyia kazi nadhani mechi ijayo tutafanya vizuri.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here