Home Kimataifa Nuksi ya Sevilla nchini Uingereza kuwaondoa Champions League hii leo

Nuksi ya Sevilla nchini Uingereza kuwaondoa Champions League hii leo

8837
0
SHARE

Rekodi zinaonesha kwamba asilimia 70 ya timu ambazo zilitoka suluhu ya bila kufungana ugenini katika mechi ya kwanza, zilifanikiwa kufudhu kwa hatua inayofuata katika michuano ya Champions League.

Kuna njaa sana ya mabao kwa Manchester United dhidi ya vilabu vya kutoka Hispania kwani katika michezo 15 kati ya United na timu za Hispania, United wameshindwa kufunga bao zaidi ya moja, wakifunga 7 katika michezo yote.

Jose Mourinho katika michezo yake 69 ya Champions League amepoteza michezo saba tu nyumbani, na katika michezo hiyo saba aliyopoteza, michezo 5 ni dhidi ya timu kutoka Hispania.

Katika hatua kama hii Manchester United wamepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya timu kutoka Hispania katika mechi zao 9 zilizopita na ilikuwa mchezo wao vs Real Madrid msimu wa 2012/2013.

Ni Barcelona tu (mabao 2) ndio ambao wameruhusu nyavu zao kuguswa mara chache zaidi katika msimu huu wa Champions League kuliko Manchester United ambao wameruhusu mabao 3.

Sevilla wanaelekea katika mchezo huu wakiwa na mkosi nchini Uingereza kwani katika michezo yao minne nchini humo hawajawahi kupata ushindi, wakiwa wametoka suluhu mara tatu na kusuluhu mara moja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here