Home Kimataifa Manchester United “Out” Champions League

Manchester United “Out” Champions League

8531
0
SHARE

Mtaani wanaiiita Mwantesa United kutokana na matokeo yasiyoeleweka ya klabu hiyo, na jina hilo limeendelea baada ya usiku wa leo mashetani hao wekundu kuondolewa katika michuano ya Champions League.

Hakuna aliyetaraji kutokana na uwezo mkubwa wa United na rekodi mbovu ya Sevilla nchini Uingereza lakini tangu dakika ya kwanza mpira ulianza kuonekana kama unawaelemea United walikua wakicheza kawaida sana.

Ni Wissam Ben Yedder raia wa Ufaransa akitokea benchi dakika ya 72 na dakika 2 baadae aliweka mpira nyavuni kabla ya dakika ya 78 kuwaua United bao la pili huku la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Romelo Lukaku.

Ben Yedder anakuwa na mabao 8 kwa sasa Champions League na sasa mabao yake 8 yanamuweka kama mfungaji namba mbili katika Champions League akiwa na mabao 4 nyuma ya kinara Cristiano Ronaldo.

Katika mchezo mwingine uliopigwa usiku huu Eden Dzeko aliivusha As Roma kwenda robo fainali baa ya kufunga bao pekee mbele ya Shakhtar Donetski, Roma wamefudhu kwa faida ya bao la ugenini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here