Home World Cup Huku Pogba, Pale Ozil, Kule Coutinho

Huku Pogba, Pale Ozil, Kule Coutinho

5291
0
SHARE

Bombardier la Urusi

Na Priva ABIUD

Mkumbukeni sana Dunga alipomuacha Neymar na Ronaldinho Gaucho, mkumbukeni vyema Raymond Domenech alipomgomea Karim Benzema, Samir Nasri, Ben Arda na Mathieu Valbuena pamoja na Yann M’villa kwenda Kombe la Dunia. Ifuatayo ni orodha kuonesha upana wa vikosi ambayo baadhi ya makocha wa timu kubwa wataamua wenyewe nani aende nani aangalie kwenye Tv.

Ufaransa

Kwenye kombe la dunia la mwaka 2014, walikwenda na viungo 9. Msimu huu kuna ongezeko kubwa la viungo wa katikati wapya. Yupo Paul Pogba, Blaise Matuidi, N’golo Kante, na Geoffrey Kondogbia. Hapa huenda mwalimu asipate tabu sana. Viungo wachezeshaji ni kama Vile Andrea Rabiot, Corentino Tolliso, Mousa Sissoko, Tiemoue Bakayoko na Yohan Cabaye (hapa kwakweli mhh akili kumkichwa). Viungo wa pembeni yupo Kingsley Coman, Florian Thauvin, Ousmane Dembele, Anthony Martial, na Thomas Lemar. Viungo washambuliaji ndio haswaa wameshiba, Anthonio Griezmann, Kevin Gameiro, Kylian Mbappe pamoja na Nabir Fekir. Kwa bidhaa hizi Ufaransa mnataka nini zaidi ya Kombe la dunia? kazi kwenu.

Uhispania

Ukizungumzia taifa lenye viungo mafundi duniani basi huwezi kuacha kuwataja watoto wa kihispaniola. Dimba la kati bila shaka Sergio Busquets hawezi kukosekana. Javier Martinez nae yumo, bila kumsahau Saul Niguez. Dimba la kati kuna wapishi kama Koke, Cesc Fabregas, David Silva, Thiago Alcantara, Ander Herrera (ingawa nina wasiwasi nae), sina uhakika sana kuhusu Illaramend kupata nafasi. kushoto yupo Juan Mata (nae amekua na msimu wa kusuasua), kulia yupo Marco Assensio (ni ngumu sana kuachwa), bila kumsahau Pedro Rodriguez. Sina uhakika na tiketi za hawa jamaa kwenda Russia (Lucas Vasquez, Vitolo, Nolito, Jonathan Vierana) na Suso kwa kiwango bora alichoonesha Ac Milan sijui ataangaliwa vipi. Viungo washambuliaji, Andreas Iniesta huyu lazima ndani, Isco nae Ndani. Itategemea wao watakavyoamua lakini shughuli ipo kwenye kungo cha kati.

Brazil

Hapa sijui nianzie wapi niishie wapi (kuna shia Brazil). kuna uwezekano wote wakaanza Fernandinho na Casamero kwenye dimba la chini. Hawa waliopo china (Renato Augusto, Ramirez na Oscar). Oscar yeye amesema hawezi kuja kuishi maisha ya kimaskini uzeeni kisa anaogopa kutokuitwa timu ya taifa kwenda kombe la dunia. Kwa kauli sioni tiketi yake. Nina wasiwasi sana kwenye nafasi ya kiungo mchezeshaji. Huenda tukaona majina mapya hapa kwa mfano kiungo chipukizi wa Hamburg Walace anawezwa kuitwa, Arthur wa Gremio mwenye miaka 21 anaweza akaitwa, tusishangae kumuona Diego ambaye anaitumikia Flamengo licha ya kwamba ana umri wa miaka 33 nae akajumuishwa. Guilane anayekipiga Fernabache huenda nae akapata nafasi licha ya kucheza michezo mitatu tu kwa timu ya taifa mwaka 2017. Hii ni kutokana na wachezaji wengi kukimbilia mabenki huko China. Viungo washambuliaji waliopo ulaya kwenye timu kubwa ni Philipe Coutinho, Willian, Paulinho na Douglas Costa. Hata hivyo Brazil sio haba watakuwa vizuri lakini mwalimu hatopata tabu kutangaza kikosi chake. Samahani nilimsahau Neymar. Lucas Moura amekimbilia Tottenham tuone nae atapata wapi upenyo

Ujerumani

Ni wazi kariba ya watu kama Bastian Schweinsteiger na Michael Ballack wasiwepo tena. Lakini kila ngoma na mdundo wake. Awamu hii sio haba sana, kati atakuwepo Emre Can, Toni Kroos, Sami Khedira, Julian Weigl, na Ilkay Gundogan. Watakaounganisha safu ya ushambuliaji wapo Leon Goretzka, Mario Gotze, Mesut Ozil, Sebastian Ruddy, Serge Gnabry. Pembeni yupo Leroy Sane, Marco Reus, Andre Schurrle, Thomas Muller, na Julian Draxler. Kazi kwake Joachim Low. Sehemu hii ya kiungo ujeruman wameshiba vyema na mwalimu atakuwa na uchaguzi huru na hawezi kujutia kukosa Fulani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here