Home Kitaifa Yanga wame-balance mzani

Yanga wame-balance mzani

9760
0
SHARE

Ushindi wa Yanga 3-1 dhidi ya Stand United umeipa Yanga pointi tatu ambazo zinaifanya ifikishe pointi 46 na kuifikia Simba licha kwamba wekundu wa Msimbazi wanaendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli.

Yanga imecheza mechi 21 mchezo mmoja zaidi ya Simba ambayo imecheza mechi 20 hadi sasa.

Kwa muda mrefu Simba iliongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba lakini Yanga wametoka nyuma na kuziba gap hilo la pointi zote. Baada ya mechi 13, Simba ilikuwa inaongoza ligi kwa pointi 29 huku Yanga ikiwa nafasi ya tano ikiwa na pointi 22.

Februari 4, 2018 Yanga ilikuwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31 wakati huo Sumba ilikuwa inaongoza ligi kwa pointi zake 38 huku kila timu ikiwa imecheza mechi 16.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Ally Ally (alijifunga) dakika ya saba, Ibrahim Ajibu akafunga goli la pili dakika tano baadaye, Obrey Chirwa ameifungia Yanga bao lililokamilisha ushindi wa Yanga. Goli pekee la Stand United limefungwa na Mayanga dakika ya 83.

Ushindi wa Yanga leo ni wa nane mfululizo katika michezo nane iliyopita kwenye ligi. Baada ya kutoka suluhu (0-0) dhidi ya Mwadui kwenye uwanja wa Uhuru, ilianza kushinda mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Januari 21, 2018 hadi leo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here