Home Dauda TV Video – Magoli yote Yanga vs Stand United Machi 12, 2018

Video – Magoli yote Yanga vs Stand United Machi 12, 2018

9313
0
SHARE

Leo Machi 12, 2018 ligi kuu Tanzania bara imeendelea kwa mchezo mmoja ambapo Yanga wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani wamepata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Stand United na kuendelea kukimbizana na Simba katika mbio za ubingwa msimu huu.

Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa taji la VPL walianza kupata goli la kwanza kutokana na beki wa Stand United Ally Ally kujkifunga wakati akijaribu kuokoa krosi ya Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajibu akafunga bao la pili dakika ya 12 na game hiyo ikaenda mapumziko Yanga ikongoza 2-0

Kipindi cha pili Stand United walifanya mashambulizi mengi na kuweka presha golini kwa Yanga lakini umakini wao mdogo katika ufungaji ndio umewakosesha magoli mengi katika mechi hiyo. Baada ya mashambulizi mengi hatimaye walifanikiwa kufungagoli dakika ya 83 kupitia kwa Vitalis Mayanga lakini Chirwa akawamaliza Stand kwa kuifungia Yanga bao la tatu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here