Home Kitaifa Singida United pumzi inakata?

Singida United pumzi inakata?

6754
0
SHARE

Sare ya Singida United 0-0 Ndanda FC Machi 11, 2018 kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida imeishusha timu hiyo kutoka nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi hadi nafasi ya 5 baada ya ushindi wa Tanzania Prisons 2-1 Mtibwa Sugar, kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Singida imefikisha pointi 36 sawa na Tanzania Prisons huku timu hizo zikiwa zimecheza mechi 22 kila moja lakini Prisons ina wastani mzuri wa magoli yanayoifanya ikae nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi juu ya Singida.

Ikifundishwa na kocha wa zamani wa Yanga Hans van Pluijm, Singida ilianza ligi vizuri raundi ya kwanza na kuwa miongoni mwa timu ambazo zilikuwa zikiwania ubingwa lakini kadiri siku zinavyosogea mbele, timu hiyo imekuwa ikirudi nyuma.

Singida United ni miongoni mwa timu nne ambazo zina idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni ikiongozwa na Simba, Yanga pamoja na Azam lakini matokeo ya hivi karibuni yameitoa kwenye mbio za ubingwa wa ligi.

Hadi sasa Singida imecheza mechi 5 mfululizo bila kushinda, mara ya mwisho Singida ilishinda 2-1 ugenini dhidi ya Mbao Februari 7, 2018 tangu hapo imepoteza mechi mbili na kutoka sare mechi tatu.

  • 11/02/2018 Singida United 0-1 Stan United
  • 17/02/2018 Kagera Sugar 1-1 Singida United
  • 03/03/2018 Azam 1-0 Singida United
  • 07/03/2018 Singida United 1-1 Ruvu Shooting
  • 11/03/2018 Singida United 0-0 Ndanda

Singida United inahitaji kufanya kazi ya ziada ili kufanikisha kumaliza katika nafasi za juu za msimamo wa ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here