Home Kimataifa Raisi wa timu aingia uwanjani na bastola kumtishia muamuzi

Raisi wa timu aingia uwanjani na bastola kumtishia muamuzi

6581
0
SHARE

Hii imetokea nchini Ugiriki ambapo raisi wa klabu ya soka ya PAOK Solanika Ivan Savvides kuingia uwanjani huku akiwa na bastola kwa lengo la kwenda kumtisha muamuzi wa mchezo huo.

Dakika ya 89 ya mchezo timu ziki 0-0 klabu ga PAOK walipafa bao na muamuzi akalikataa akidai ni offside, hali hii haikukubalika katika benchi la PAOK na ndipo raisi wa klabu hiyo aliingia uwanjani.

Wachezaji wa timu pinzani ga AEK Anthens waliamua kuondoka uwanjani baada ya tukio hilo wakidaiwa kuhofia usalama wao kwani mashabiki wa PAOK nao walikuwa wameanza kukasirika sana .

Ilimbidi muamuzi wa pambano hilo kusimamisha kwanza mchezo huo na baada ya muda aliamua kuahirisha mchezo huo ikimaanisha kwamba mchezo huo umeisha kwa sare ya nunge nunge.

Savvids aliwahi kuwa mbunge nchini Ugiriki na ni moja kati ya watu wanaotajwa kumiliki pesa nyingi sana nchini Ugiriki japo suala hili linaweza kumuweka matatizoni yeye pamoja na timu yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here