Home Kitaifa Mechi 6 Mbao bila ushindi

Mechi 6 Mbao bila ushindi

4555
0
SHARE

Usiku wa Machi 11, 2018 Mbao FC ilipoteza mchezo wa nne mfululizo ugenini baada ya kufungwa 2-1 na Azam kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.

Matokeo hayo yanaifanya Mbao kucheza mechi sita mfululizo bila kupata ushindi kwenye ligi, mara ya mwisho timu hiyo ya mkoani Mwanza ilishinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanjabwa CCM Kirumba Februari 4, 2018.

Baada ya ushindi huo, Mbao imepoteza michezo mitano na kupata sare moja, kati ya mechi hizo sita, imepoteza mchezo mmoja na kutoka sare mechi moja nyumbani, imepoteza mechi nne ikiwa ugenini.

  • 07/02/2018 Mbao 1-2 Singida United
  • 11/02/2018 Mbao 0-0 Mtibwa Suar
  • 26/02/2018 Simba 5-0 Mbao
  • 03/03/2018 Tanzania Prisons 1-0 Mbao
  • 07/03/2018 Mbeya City 2-1 Mbao
  • 11/03/2018 Azam 2-1 Mbao

Mbao ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi, ina pointi 19 baada ya kucheza mechi 22 huku ikiwa imebakiza michezo nane kabla ya ligi kumalizika. Msimu uliopita ilishinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Yanga na kunusurika kushuka daraja katika siku ya mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here