Home Kitaifa “Kuna raha kuzifunga Simba na Yanga”-Stand United

“Kuna raha kuzifunga Simba na Yanga”-Stand United

5715
0
SHARE

Leo Jumatatu Machi 12, 2018 kutakuwa na mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Stand United uwanja wa taifa, kuelekea mchezo huo mwenyekiti wa Stand United Elson Maeja amesema kuna raha ya aina yake kupata matokeo dhidi ya timu kubwa.

“Mchezo utakuwa mzuri kwa sababu unapocheza na Simba na Yanga kuna raha yake na kuna raha ya kuzifunga kwa sababu ni timu ambazo zina sifa.”

“Wachezaji wetu wanapenda kucheza na hizo timu kwa sababu wanaonesha viwango vyao na kujitangaza na kusajiliwa”

Machi 2, 2018 Stand United iliilazimisha sare Simba kwenye uwanja wa taifa kwa kufungana magoli 3-3.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here