Home Kitaifa Rais wa Simba kazungumzia maendeleo ya uwanja Bunju

Rais wa Simba kazungumzia maendeleo ya uwanja Bunju

14546
0
SHARE

Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah ‘try again’ amezungumzia suala maendeleo ya uwanja wao wa kufanyia mazoezi na namna ambavyo mipango yao ilivyo pamoja na club licensing kwa nama walivyoweza kufikia vigezo.

“Klabu ya Simba ina eneo lake pale Bunju na huko nyuma tuliwahi kuagiza nyasi za bandia lakini kwa bahati mbaya zimekwama bandarini, tunafanya jitihada kubwa ili kuzigomboa nafikiri ndani ya mwezi huu nyasi hizo tutakuwa tumezitoa ili kuweza kuendelea na ujenzi wa uwanja wetu.”

“Kwenye mkutano mkuu uliopita mwekezaji wetu aliahidi kwamba atatengeneza viwanja (vya nyasi za asili na nyasi bandia) kwa hiyo nataka niwaahidi kwamba upande huo umekaa vizuri, wapenzi na wanachama wasiwe na shaka katika hilo. Ndani yamiezi miwili tutakuwa tumekamilisha kwa sababu maandalizi ya eneo lile yalishakamilika ni kutandika tu zile nyasi lakini miundombinu mingine tunahitaji muda kidogo tuweze kuikamilisha lakini niseme kufikia mwaka ujao mambo yote haya yatakuwa sawa.”

Uongozi wa Simba umesema hauna shaka katika suala la club licensing kwa sababu vigezo vyote wameweza kuvifikia.

“Simba tumetimiza masharti yote ya club licensing kwa maana tunayo timu ya U17, U20 na tumeshaanza mchakato wa U14 kwa hiyo katika eneo hilo tuko vizuri kwa sababu hata viwanja vyetu tumesajili uwanja wetu ni uwanja wa Taifa kwa sababu eneo hilo halisemi uwe na uwanja wako wanataka uwe na kiwanja cha mazoezi ambao unaweza ukawa wakukodi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here