Home Kitaifa Mbeya City wanafahamu leo tutawapapasa”-Masau Bwire

Mbeya City wanafahamu leo tutawapapasa”-Masau Bwire

6270
0
SHARE

Ligi kuu Tanzania bara inaendele leo Jumapili Machi 11, 2018 kwa michezo mitano kupigwa kwenye viwanja tofutti.

Ruvu shooting watakuwa nyumbani kuikaribisha Mbeya City kwenye uwanja wa mabatini, mlandizi mkoani pwani. Kuelekea mchezo huo, afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema, ni zamu ya Mbeya City kupapaswa.

“Walimu wamenihakikishia kwamba tutaendelea na ka-mfumo ketu ka ‘papasapapasa’, zamu ya Mbeya City imefika na kwa sababu wanajua huku wanapokuja ni kupapaswa naamini watakuwa wamejipanga kwa ajili ya kupapaswa na lazima tuwapapase kwa sababu tunahitaji matokeo ili malengo yetu yaweze kutimia.”

“Ni siku ambayo tumejipanga na wao wanajua hivyo tunataka kuwapapasa hata wao pia nina hakika wamejipanga kuapapawa kwa sababu wanaijua Ruvu Shooting ya sasa kwamba kasi yake ni ya hatari na uwazo wake ni mkubwa sana, watake wasitake watapapaswa.”

Kinachonipa matumaini ni ubora wa timu yetu, katika timu zenye uwezo wa kucheza mpira kwa ubora zinanazoshiriki ligi kuu tanzania hii, huwezi kutaja timu tatu bila kuitaja Ruvu Shooting. Jambo la pili ni morali ambayo wanayo vijana, nimeongea na baadhi ya wachezaji wakaniambia bado wanahitaji kutoa faraja kwangu kwa kuondokewa na mama yangu.

Ratiba ya mechi nyingine zinazochezwa leo Machi 11, 2018

  • Azam FC vs Mbao FC (Azam Complex-Chamazi, Dar)
  • Singida United vs Ndanda FC (Namfua-Singida)
  • Majimaji FC vs Lipuli FC (Majimaji-Songea)
  • Tanzania Prisons vs Mtibwa sugar (Sokoine-Mbeya)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here