Home Kimataifa Mbeleko iliwasaidia United kuizima Liverpool

Mbeleko iliwasaidia United kuizima Liverpool

7003
0
SHARE

Mara ya mwisho kwa Manchestee United kupata ushindi mara 20 katika michezo yao 30 ya EPL ilikuwa msimu wa 2012/2013 kipindi hicho kocha alikuwa SAF,na ushindi wa jana mbele ya Liverpool umewapa ushindi wa 20 katika mechi 30.

Goli pekee la Liverpool linawafanya United kuruhusu bao 2 tu katika michezo yao 14 Old Traford msimu huu, huku Rashford akifunga mabao 2 kwa mara ya kwanza tangu afanya hivyo vs Arsenal 2016.

Lakini kuna matukio ambayo yanaleta mjadala mkubwa kuhusiana na mchezo huo, faulo ya Rashford kwa Milner ilipaswa kuwa kadi ya pili ya njano japo muamuzi Craid Pawson alimpa njano ya kwanza.

Lakini njano ya kwanza jwa Rashford ilikuwa pale alipofunga bao la kwanza, kitendo cha kwenda kujirusha kwa mashabiki wakati akishangilia bao hilo ilikuwa kadi lakini muamuzi alikausha.

Hakuishia hapo Rashford alimchezea rafu mbaya Alexandre Arnold na ilikuwa kadi ya wazi iliyokuwa ikimshuhudia Muingereza huyo nje ya uwanja lakini bado muamuzi hakufanya hatua yeyote kwa Raahford.

Kuna tukio ambalo Ashley Young alionekana wazi kwamba kulikuwa na contact kati yake na Salah katika eneo la penalty box na Young alionekana kumuangusha Salah lakini muamuzi hakutoa penati.

Beki wa kulia wa Manchester United Antonio Valencia aliunawa mpira wazi wazi uliopigwa na Andrew Robertson lakini wapi, muamuzi hakuona hilo na wala hakutoa penati katika tukio hilo.

Yapo matukio mengi ikiwemo tukio la Fellaini kumuangusha Sadio Mane kwenye eneo la 18 na refa akapeta, tukio la Antonio Valencia teke la kifua kwa Sadio Mane, United waliibuka kidedea bao 2-1 na sasa wanaanza kuwa na uhakika kumaliza katika nafasi ya pili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here