Home Kimataifa HATARI “PSG waliwaambia polisi wasiwalinde Real Madrid”

HATARI “PSG waliwaambia polisi wasiwalinde Real Madrid”

7266
0
SHARE

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, imebainika kwamba wakati wa mchezo wa marudiano kati ya Paris Saint German dhidi ya Real Madrid wenyeji wa mchezo huo hawakutaka wageni wapewe ulinzi na polisi.

Ni kawaida kwamba katika mechi kubwa na kunapokuwa na wachezaji wenye majina makubwa huwa kunakuwa na polisi ambao huongoza msafara wa timu kwa ajili ya usalama wa wachezaji.

Msafara wa basi la timu huongozwa na pikipiki pamoja na magari ya polisi, lakini gazeti moja la michezo nchini Ufaransa limedai kwamba maofisa wa PSG walifanya mpango Real Madrid wasipewe ulinzi wakati wakielekea uwanjani.

Inadaiwa kwamba moja ya maofisa wa juu kabisa katika klabu hiyo aliwaambia polisi kwamba wawaacha Madrid watoke peke yao kwenda uwanjani Parc Des Princes japo haikufahamika kwanini alitaka hivyo.

Polisi nchini Ufaransa hawakufanya kile ambacho PSG walitaka, japo jambo hili linaonekana linaweza kuleta mjadala mkubwa na tayari UEFA wameshapata taarifa kuhusu jambo hili na wameanza kufanya uchunguzi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here