Home Kimataifa Zlatan aamua kuachana na soka atafutwa kwa wizi

Zlatan aamua kuachana na soka atafutwa kwa wizi

13243
0
SHARE

Hii ni historia kwa kina kuhusiana na Maisha ya Zlatan Ibrahimovic.

Imeandaliwa na Priva ABIUD

Sehemu ya kwanza

Zlatan anaamini kucheza soka kwake ni kama kufanya ibada. Kiujumla mpira aliuchukulia kama dini. Johnny Gyllensjoa anakiri kuwa mwanzoni ilimuia vigumu sana kumpokea Zlatan katika klabu ya Malmo FF. asubuhi moja tulivu Mwaka 1996 Zlatan aliwasili mazoezini asubuhi na mapema. Alipofika mazoezin alikutana na mzee mmoja mwenye mvi nyingi kama pamba za mwanza. Mzee huyu alikuwa Kocha wa vijana wa Malmo. Mazungumzo yao yalichukua dakika 90. Mzee Johnny Gyllensjoa alimchokonoa sana Zlatan ili kugundua malengo yake hasa yalikuwa ni nini. Zlatan alikuwa na majibu ya haraka na mbaya zaidi mafupi. Kiufupi tunaweza kusema alikuwa na majibu “shombo”

Mzee Johnny alimkazia macho Zlatan lakini kwakuwa Zlatan alikuwa na nyodo wala hakupepesa macho. “Nakumbuka moja ya jina alilotaja ilikuwa ni Ronaldo De lima tu. Wakati Fulani mazoezini alikata tama. Siku nyingine alikuwa hafiki mazoezini hata wiki nzima. Baadae alitafutiwa mtaalamu wa saikolojia ili kumsaidia” alisema Mzee Johnny.nJohnny aliuabudu sana mpira, pamoja na kwamba alikuwa akicheza klabu kubwa kama Malmo FF bado alitumia muda wa zaida kucheza vilabu vya mtaani kwao. Kuna wakati timu yake ya Malmo ilikuwa inacheza Jumamosi, jumapili yake yeye alikwenda kucheza soka kwenye klabu ya Rosengard ya mtaani kwake.

Alikuwa anacheza soka kila siku. Walimuwa wake alisema Zlatan kichwa chake alikuwa anafanya mambo yake kama mvuta bangi; alikuwa haupi mwili wake muda wa kupumzika kwa kuamini kuwa kucheza kila mara kungeimarisha mwili wake bila kujali afya yake na ufanisi mzuri wa misuli ya mwili.

Maisha na Familia yake

Kama ilivyo kawaida mpira wa miguu ni biashara au kazi ya watoto waa watu masikini; ndivyo ilivyokuwa kwa Zlatan Ibrahimovic ambaye alilelewa katika makuzi ya kimasikini. Ilikuwa shughuli kwa Zlatan kupata viatu vya kucheza mpira. Mwalimu wake anadai ilikuwa ukimuona Zlatan na viatu vipya, jua kuna mtu kashalizwa huko. Wazazi wa Zlatan walikuwa wazururaji wa mataifa tofauti waliokutana nchini Sweden katika harakati za kutafuta riziki; mzazi mmoja kutoka Bosnia (Baba) na Mama yake alikuwa ni raia wa Croatia. Zlatan alipitia kipindi kigumu sana baada ya mama yake na Baba yake kupeana talaka akiwa na miaka miwili tu. Hali ile ilimuathiri sana katika ukuaji wake.

Alijizolea umaarufu mkubwa sana shule kwa sababu ya wizi na ukorofi wa kupindukiaAmesalimika mara kadhaa kwa tuhuma hizo hizo. Faida kubwa aliyokuwa nayo shuleni licha ya ubabe wake na wizi ni soka. Alipendwa sana kwa kiwango chake maradufu.

Alikuwa akisafiri kilometa 5 kila siku kwenda kwenye kiwanja cha Malmo kwa ajili ya majaribio kwa kutumia baiskeli ambayo nayo ilisemekana aliiba.

Marafiki zake wengi walikuwa hawapendi mazoea nae kwa vitendo vyake vya kuchukua vitu vyao kwa fujo. Hakuwahi kuishiwa vimbwanga, siku moja join baada ya mazoezi aliondoka na baiskeli ya kocha wake Bw. Ola Gallstad bila rihaa yake. Wachezaji wenzake walishangazwa sana na kitendo kile cha kijasiri kwani mwalimu wao alikuwa mkorofi sana. Hata kesho yake alipoirejesha hakuomba radhi alisema tu bahati mbaya. Aliwahi kutafutwa na polisi kwa kusadikika kuwa aliiba baiskeli kwenye kituo kimoja cha polisi mjini Malmo.Zlatan aliacha kabisa kucheza mpira na kwenda kuuza nguo katika moja ya masoko maarufu huko Malmo. Kwa mara nyingine kocha huyo wa timu ya vijana alimsihi sana zlatani.

Zlatani alikuwa hapendi kukosa magoli, na hili lilimfanya ajione butu na kumkatisha tamaa. Kocha wake alimwambia kukosa magoli ni sehemu ya kazi yake. Alimpelekea tepu za De Lima na vijarida vingi sana kutaka kumtia hamasa. Ushawishi mkubwa wa Bw. Johnny Gyllensjo ndio ulimfanya Zlatan kuvaa jezi ya Ajax, Barcelona, inter Milan, Ac Milan, PSG na Man United. Usikatae sauti za wanaokusuma usonge mbele.

.

Itaendlea usikose makala ijayo…

.

Sehemu ya pili

ZLATAN APIGANA UWANJANI, ADAI ANAMPENDA MAMA KULIKO BABA

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here