Home Kimataifa Mourinho amfumua Klopp

Mourinho amfumua Klopp

9463
0
SHARE

 

Kwa takribani miezi mitatu Rashford hakupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Man United. Hatimaye siku yake atakuwa mchezaji pekee ataketamkwa zaidi kwa kuwainunua kimasomaso mashabiki ugani Old Trafford. Liverpool imepata kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa mashetani wekundu

Kwa taarifu tu ni kwamba magoli yote yamefungwa wa wachezaji wa Man United baada ya Erick Baily kujifunga. Safu ya ushambuliaji ya Liverpool imeshindwa kabisa kufanya kile walicho stahili kukifanya.

 

TAKWIMU ZA MCHEZO  

Timu Man United Liverpool
Mashuti 6 12
Pasi 281 585
Kutibua mipango 24 7
Kuondoa mipira ya juu 16 12
Makosa/adhabu 10 16

 

Liverpool walitawala mchezo kwa asilimia 68 dhidi ya yasilimia 32 za Man United. Kwa matokeo haya Man United inasogea nafasi ya pili kwa tofauti ya alama 5 wakiwa na alama 65 liverpool akifuatia kwa alama 60 wakiwa wamecheza michezo 30 pekee. Kwenye michezo mitano ya mwisho ya Liverpool waliruhusu goli moja tu hali iliyofanya baadhi ya mashabiki kuamini kuwa tatizo la ulinzi limeisha lakini katika mchezo wa leo huenda lugha ikawa tofauti.

Kauli za makocha

  Mourinho “kipindi cha kwanza tulikuwa na njaa sana, tulihitaji kutawala mchezo kwa kutumia nafasi kila mara tulipozipata. Kikubwa wapinzani wetu hawakuwa makini. Kipindi cha pili haikuwa lengo letu kuzuia sana, ila Liverpool waliturudisha nyuma sana kwa sababu walikuwa wanahitaji ushindi wa lazima. Walikuja kwa fujo mno kitendo kilichotufanya tuzuie. Haijalishi tumecheza vibaya kivipi, ushindi ndio lengo la msingi na linaleta furaha kuliko anayecheza vizuri kisha anafungwa”

Klopp “ilikuwa bahati mbaya sana kuwa nyuma ya Man United magoli mawili. Nilijua tayari mpira umeisha, nilisibiri tu kuona watakosea wapi. Lukaku ni mchezaji mzuri sana, kila mara tulimlinda zaidi yeye, hatukuwaza sana kama Rashford angetuumiza mara mbili. Tulipata nafasi ya kupiga mashuti ya mbali lakini hatukufanikiwa sana. Fellain alicheza faulo mbaya kwenye boksi na kila mtu aliona wazi ni penati.

Takwimu muhimu

 

Man United imeifunga Liverpool mara 68, rekodi pekee ambayo Liverpool imefungwa mara nyingi zaidi kuliko klabu yoyote.

Man United imeweza kuvunja rekodi yake ya kushinda michezo 20 kati ya 30 msimu huu. Msimu wa 2017 walishinda michezo 18 kati ya 30 za mwanzo, 2016 walishinda michezo 19 kati ya 30, na mwaka 2015 walishinda 20.

Man United imelenga mashuti mawili tu kulekea golini nayo yalipigwa na Rashford tu. Lukaku sasa amefikisha asisti 7 katika ligi na kuweka rekodi yake

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here