Home Kitaifa Kocha Yanga kuhusu kiwango cha Kamusoko vs Kagera Sugar

Kocha Yanga kuhusu kiwango cha Kamusoko vs Kagera Sugar

11749
0
SHARE

Kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe Thabani Kamusoko alirejea uwanjani kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuuguza majera.

Kamusoko hakuonekana uwanjani tangu alipoumia Septemba 16, 2017 kwenye mchezo wa ligi kati ya Majimaji dhidi ya Yanga, katika mechi dhidi ya Kagera Sugar alicheza kwa dakika 71 kabla ya kupumzishwa kumpisha Yusuph Mhilu.

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema benchi la ufundi limeridhishwa kwa kiwango alichokionesha Kamusoko licha ya kuwa nje kwa muda mrefu.

“Ni mchezaji ambaye anakiwango kizuri siku zote lakini kwa vile ametoka kwenye majeraha tunaona anaendelea vizuri ndio maana tumeanza kumpa mechi na tumeridhika kwa dakika ambazo tulipanga acheze halafu tukampumzisha.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here