Home Kitaifa Baada ya kikosi cha Stars kutangazwa, “Nimejisikia vibaya”-Habibu Kiyombo

Baada ya kikosi cha Stars kutangazwa, “Nimejisikia vibaya”-Habibu Kiyombo

15635
1
SHARE

Alhamisi Machi 8, 2018 kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Morocco alitaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Algeria na DR Congo ambazo zinatarajia kuchezwa Machi 22 na 27, 2018.

Katika uteuzi huo, jina la mshambuliaji Habibu Kiyombo si miongoni mwa wachezaji wanaunda timu ya taifa licha ya kijana huyo kufanya vizuri kwenye mechi za ligi kuu.

www.shaffihdauda.co.tz imemtafuta Kiyombo na kuzungumza naye kujua namna alivyopokea uteuzi wa timu ya taifa huku yeye akiwa nje ya timu hiyo.

“Nimejisikia vibaya kwa sababu nilitamani kupata nafasi katika kikos hicho lakini sijapata. Inaumiza lakini nitajitaidi kupambana kutimiza malengo yangu kwa sababu kila mchezaji ndoto yake ni kucheza timu ya taifa”-Habibu Kiyombo.

Kiyombo amefunga magoli 9 kwenye ligi ambapo tayari Mbao imecheza mechi 21 hadi sasa. Alishinda pia tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba ligi kuu msimu huu (2017/18).

Comments

comments

1 COMMENT

  1. Kocha amekalili huu ndo muda wakutest Makinda kwaajili ya baadae Mayanga amechemka Kwanza hawezi kuunganisha timu kilamtu anacheza kwauwezo wake binafsi anabebwa na TFF yaani hata ngorongoro heroes? achenie masihara Bahama kusoma hujui hata picha?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here