Home Kitaifa Ajib ametafuta goli kwa zaidi ya dk 700

Ajib ametafuta goli kwa zaidi ya dk 700

6582
0
SHARE

Ibrahim Ajib hatimaye amevunja ukame wa magoli aliodumu nao kwa zaidi ya miezi minne baada ya kufunga bao lake la kwanza tangu alivyofunga mara ya mwisho dhidi ya Stand United Oktoba 22, 2018 kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Ajib alifunga magoli mawili kwenye mchezo dhidi ya Stand United wakati Yanga iliposhinda kwa magoli 4-0, tangu wakati huo alikuwa kwenye wakati mgumu wa kutofunga katika mechi tisa (9) zilizopita.

Amefunga goli moja kati ya matatu wakati Yanga ikishinda 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa. Ajib aliifungia Yanga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati na kufuta ukame wake ambao ulidumu kwa zaidi ya dakika 700.

Magoli mengine yamefungwa na Yusuph Mhilu huku goli la tatu likitokana na mchezaji wa Kagera Sugar Juma Shemvuni.

Yanga imefikisha pointi 43 baada ya mechi 20 hivyo kurudi katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa kuitoa Azam ambayo ina pointi 41 ikiwa imecheza mechi 21. Simba bado inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.

Jumatatu Machi 12, 2018 Yanga itacheza mchezo wa ligi dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here