Home Kimataifa Zimwi la mkosi laziandama timu za London

Zimwi la mkosi laziandama timu za London

5956
0
SHARE

Tofauti na wengi walivyotarajia kwamba EPL inaweza kuingiza timu nne katika robo fainali, uzoefu umeeaondoa Tottenham katika mashindano ya Champions League na sasa Juve anakwenda robo fainali.

Hili ni tatizo, japo tatizo kubwa linaonekana kwa timu za EPL kutoka ukanda wa London ambako ndiko zinakopatikana timu kubwa tatu pale Uingereza Tottenham, Chelsea pamoja na Arsenal.

Tayari timu moja kubwa kutoka London imeondolewa mashindanoni, Chelsea nao hawana uhakika wa kufudhu kutokana na suluhu ya moja moja waliyoipata katika mechi ya kwanza nyumbani vs Barcelona.

Tottenham kabla ya mchezo wa jana ilikuwa kati ya timu tatu ambazo hazijawahi kuonja kipigo katika michuano hiyo nyingine zikiwa Liverpool na Barcelona lakini jana wamepokea kipigo pekee na kimewatoa mashindanoni.

Leo tena timu nyingine ya London iko majaribuni, ni Arsenal ambapo hii leo watakuwa wenyeji wa Ac Millan huku matokeo ya klabu hiyo katika hatua kama hii michuano ya Ulaya ikiwa sio nzuri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here