Home Kimataifa Wachezaji Simba wagomea sub ya Kichuya

Wachezaji Simba wagomea sub ya Kichuya

10875
0
SHARE

Wachezaji wa Simba waligomea mabadiliko yaliyokuwa yanafanywa na benchi la ufundi kutaka kumtoa Shiza Kichuya ili nafasi yake aingie Laudi Mavugo.

Wakati Simba wakiwa nyuma kwa goli 1-2 dhidi ya waarabu Al Masry, benchi la ufundi la wekundu wa Msimbazi lilitaka kumuingiza Mavugo ili aongeze nguvu kwenye safu ya ushambuliaji akishirikiana na Bocco pamoja na Okwi.

Kibao kilivyoonekana kikimuita nje Kichuya, haraka wachezaji wa Simba walikimbia na kumzuia Kichuya asitoke nje ya uwanja kisha walionekana wakijadili jambo na kocha wao msaidizi Masoud Djuma.

Baada ya muda mfupi kibao kikanyanyuka tena na safari hii aliyekuwa anakwenda benchi alikuwa ni John Bocco  kumpisha Mavugo.

Badika chache baadaye Simba wakafunga goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati ulipigwa na Emanuel Okwi na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa 2-2.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here