Home Kimataifa Sergio Ramos ndio mchezaji mhuni kuliko wote waliowahi kucheza Champions League

Sergio Ramos ndio mchezaji mhuni kuliko wote waliowahi kucheza Champions League

13892
0
SHARE

Wakati wakina Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanashindana kuweka rekodi za mabao na kufanya mambo mazuri katika soka, hali ni tofauti kwa mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos kwani anaweka rekodi za kihuni.

Rekodi zinaonesha Ramos ndio beki ambaye anacheza rafu mbaya zaidi katika ligi ya soka nchini Hispania La Liga suala ambalo limewalazimu waamuzi katika ligi hiyo kumpa kadi nyekundu 19.

Hakuna mchezaji yeyote tangu La Liga ianze ambaye amewahi kupewa kadi nyekundu kama ambavyo Sergio Ramos amepewa na ndio anashikilia rekodi ya kadi nyingi nyekundu katika michuano hiyo.

Ukiacha ufalme huo wa kadi alionao Ramos katika La Liga, sehemu pekee ambayo Ramos alikuwa amebakisha ni Champions League ambako huko Paul Scholes ndio alikuwa akishikilia rekodi ya kadi za njano akiwa na 36.

Lakini sasa Ramos amekaa juu ya Scholes kwani baada ya mchezo vs PSG sasa Ramos anakuwa na jumla ya kadi za njano 37 idadi ambayo hakuna mchezaji yeyote Champions League ambaye amewahi kupewa kadi nyingi za njano kama Ramos.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here