Home Kimataifa Hivi ndivyo Gennaro Gattuso alivyoibadilisha “La Scala del Calcio” kuwa machinjio

Hivi ndivyo Gennaro Gattuso alivyoibadilisha “La Scala del Calcio” kuwa machinjio

10589
0
SHARE

“Mpira hujiandai na kushinda tu kiakili wala kisaikolojia, huwa unapaswa kujiandaa kimwili, kinguvu na kiakili” hiyo ilikuwa kauli ya kwanza wakati Gennaro Gatuso anapewa kuinoa Ac Milan mwezi November mwaka jana.

Kauli hii unaweza kuichukulia kirahisi lakini Gattuso alimaanisha mengi, suala la kimwili Gattuso alimaanisha nguvu na toka ameichukua timu Milan wanaonekana kuimarika zaidi pysically 

Wakati Vincenzo Montella alipokuwa kocha mkuu wa timu ya Ac Milan, Milan walikuwa wana tatizo kubwa la stamina na sikuwa nashangaa wao kuruhusu mabao mengi katika dakika za mwisho.

Milan ya Montella walikuwa wakikimbia kwa wastani wa kilomita 103 kwa kila mchezo katika Serie A lakini tangu Gattuso aichukue Milan timu imetoka kutoka kukimbia kilomita 103 hadi kukimbia kilomita 114 kwa mchezo.

Watu wengi hawakuwa na imani na Gattuso wakati anapewa Ac Milan haswa suala la kimbinu, wengi waliona ni mtu ambaye asingeleta mabadiliko makubwa ndani ya Ac Milan haswa kuhusu suala la mfumo.

Montella alikuwa muumini mkubwa wa 3-4-2-1 mfumo ambao ulikuwa unamfanya moja kati ya walinzi wa kati bora duniani Leornado Bonucci kuonekana sii lolote uwanjani haswa kutokana na utumwa aliokuwa anapata katika mfumo huu.

Gattuso alichofanya baada ya kuichukua timu aliswitch kutoka 3-4-2-1 ya Montella na kuipeleka kwenye 4-3-3 mfumo ambao hadi Silvio Berlusconi (mmiliki wa zamani wa Ac Milan) alisema anahisi maumivu ya tumbo kila akiuona mfumo huu.

Tangu Gattuso aibadilishe Milan hadi kwenye kucheza 4-3-3 Leornado Bonucci ameanza kuonekana kama Bonucci yule aliyekuwa Juventus na muunganiko wake na Alessio Romagnoli unaifanya defence ya Milan kuwa kati ya defence bora Serie A kwa sasa.

Eneo la ulinzi la Ac Milan ndio linawafanga hadi hivi sasa wawe wamecheza michezo 13 bila kupoteza mchezo hata mmoa na usalama wao katika eneo hili umewapa clean sita mfululizo katika michezo yao ya mwisho(mara ya mwisho Milan kucheza michezo mingi hivi bila kupoteza ilikuwa 2009/2010).

4-3-3 Gattuso amempa Lucas Rodrigo Biglia uhuru wa kulinda eneo la kiungo na hii imewafanya viungo wa pembeni wa Milan Bonaventura na Franck Kessie kucheza kwa uhuru zaidi na kuiendesha timu mbele na hii inamfanya Kessie kuwa kati ya wachezaji bora Serie A tangu apewe timu Gattuso.

Namna ambavyo Gattuso ameweza kuifanya Milan iswitch mfumo kutoka 4-3-3 hadi 4-1-4-1 pale timu ikishambuliwa ninnamna nyingine ambayo inamfanya Gattuso kuonekana kama moja ya makocha ambao wako flexible katika kunyumbua mifumo.

Tayari sio watu wa Milan tu bali na Waitalia wengi Gattuso ameanza kupenya mioyoni mwao huku pia akipewa sifa kwa jinsi anavyompa nafasi Patrick Cutrone dogo ambaye anatajwa kama Inzaghi ajae nchini Italia.

Andriy Shevchenko ameshatuma salamu kwa mzee Arsene Wenger na kumuonya kuhusu aina ya Milan anayokwenda kukutana nayo, huku Chenko akionya kwamba Milan hii inaonekana kama ile Milan yao.

Ni La Scala del Calcio aka San Siro hapa ndipo ambapo mzee Wenger na skills zake atakwenda kukutana na Gattuso aliyeko fiti kimbinu, kiakili na kinguvu, hapa ndipo Wenger anaweza kuendelea kuwaumiza Arsenal.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here