Home Kimataifa Barcelona watabeba La Liga, lakini wanaweza kuvunja rekodi hizi?

Barcelona watabeba La Liga, lakini wanaweza kuvunja rekodi hizi?

7882
0
SHARE

Tayari iko wazi kwamba Barcelona wana nafasi kubwa kutwaa La Liga msimu huu, kuwapiga Atletico Madrid ambao ndio walionekana kama tishio kwao msimu huu kumewaweka vizuri sana kubeba La Liga.

Hadi sasa miamba hiyo ya Catalunya haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza?

Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho.

Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994).

Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano.

Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep Gurdiola ya michezo 31 bila kufungwa (2010/2011), lakini Barca wana kazi kuifikia rekodi ya Real Sociedad (1979/1980) kucheza michezo 38 bila kupoteza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here