Home Dauda TV Video-Zimetajwa sababu Yanga kupoteza taifa, kocha anamatumaini ugenini

Video-Zimetajwa sababu Yanga kupoteza taifa, kocha anamatumaini ugenini

8063
0
SHARE

Baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa klabu bingwa Afrika kwa kufungwa 2-1 na Township Rollers ya Botswana, kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa alizungumza na vyombo vya habari kueleza nini hasa lilikuwa tatizo hadi timu yao ikapoteza mechi ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani.

Ukiachilia mbali sababu za kupoteza mchezo zilizotajwa na Nsajigwa  amesema yanga inaweza kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa siku 10 zijazo huko Gaborone, Botswana.

“Kiujumla tatizo kubwa tulikuwa tunawaacha wanamiliki mpira kwa muda mrefu, tulikuwa tunachelewa kwenda kukaba na tulikuwa tunachelewa kurudi kurudi nyuma ili kujilinda wakati tunaposhambuliwa, hicho ndio kikubwa macho tumekiona lakini kwa namna nyingine hata sisi tunaweza kupata matokeo kwao.”

“Tumepoteza lakini hiki ni kipindi kimoja, ninaimani mechi ya ugenini tunaweza tukapata matokeo vilevile kwa sababu wao wamecheza hapa wamepata matokeo hata sisi tutarudi kujiandaa kurekebisha makosa yetu ambayo tumefanya mechi ya ugenini tunaweza kupata ushindi kama ambavyo wamefanya wao kwa sababu tumeona wanafungika”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here