Home Dauda TV Video-sare ya 2-2 Simba vs Al Masry uwanja wa taifa

Video-sare ya 2-2 Simba vs Al Masry uwanja wa taifa

8190
0
SHARE

Wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya Caf Confederation Cup ‘kombe la shirikisho Afrika’ Simba, wametoka sare ya kufungana 2-2 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya mashindano hayo wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.

Simba walianza kupata goli dakika ya 10 baada ya mchezo kuanza kwa mkwaju wa penati uliofungwa na John Bocco baada ya mlinzi wa Al Masry Mohamed Koffi kushika mpira kwenye box wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa. Goli hilo halikudumu dakika moja baadaye al masry wakasawazisha kupitia kwa Mohamed Ahmed.

Dakika ya 26 Al Masry walipata mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa simba James Kotei kuunawa mpira kwenye box, mkwaju huo wa penati ukakwamishwa kambani na Ahmed Abdalrauf lakini simba wakasawazisha kwa mara nyingine wakipata tuta baada ya Mohamed Koffi kuushika mpira wakati akijaribu kumzuia Okwi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here