Home Kimataifa Tottenham vs Juventus, nampa Tot nafasi kubwa kwenda robo fainali

Tottenham vs Juventus, nampa Tot nafasi kubwa kwenda robo fainali

5414
0
SHARE

Rekodi zinawabeba Tottenham hii leo, mechi ya kwanza ugenini walitoka sare ya mabao 2 kwa 2 na rekodi inaonesha 83% ya timu zilizotoka sare ya 2-2 ugenini zilifanikiwa kufudhu kwa hatua inayofuata ya Champions League.

Tottenham wanaelekea katika mchezo huu wakiwa bado hawajaonja machungu ya kipigo kwani hadi sasa ni Liverpool, Tottenham Hotspur na Chelsea ndio ambao hawajawahi kupoteza katika Champions League.

Katika misimu mitatu iliyopita ya Juventus wamefanikiwa kuingia fainali ya Champions League mara mbili lakini Tottenham Hotspur wenyewe wamewahi kufika robo fainali ya michuano hiyo mara moja(2010/2011).

Uwanja wa Wembley ni uwanja rafiki zaidi kwa Tottenham kwa sasa kwani katika michezo yao minne ya mwisho katika uwanja huo Spurs wamefanikiwa kushinda yote wakifunga mabao 3 kila mchezo.

Lakini Juve haogopi ugenini, michezo yao 7 ya mwisho ugenini wameshinda 3 wakasuluhu 3 na kufungwa mmoja na michezo yao ya mwisho mitatu ya ugenini wamecheza bila kuruhusu wavu wao kuguswa.

Mbinu za Maurcio Pochettino na kiwango cha timu yake haswa uwepo wa Harry Kane ambaye amehusika kwa 53% katika mabao ya Tottenham katika Champions League vinaweza kuwa sababu kubwa kwa Juventus kuishia hapa katika Champions League.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here