Home Kimataifa “Mechi ingechezwa saa 8:30 waarabu wangekaa mapema tu”-Rage

“Mechi ingechezwa saa 8:30 waarabu wangekaa mapema tu”-Rage

6588
0
SHARE

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage anaamini kama mchezo wa kombe la shirikisho Afrika kati ya Simba na Al Masry ungechezwa mchana wa jua kali basi mnyama huenda angefaidika na hali ya hewa ya joto ambayo ingewasumbua wapinzani wao kwa sababu wanatoka ukanda wa wenye baridi.

Rage amesema kipindi cha nyuma Simba walipata matokeo kwenye michezo mingi ya nyumbani kwa kutumia mbinu hiyo ya kuwachezesha waarabu kwenye jua kali.

“Bado nasikitika sana kwa jinsi nilivyoona Simba wamecheza vizuri, kama mpira ungechezwa saa 8:30 au saa 9:00 mchana wale waarabu walikuwa wepesi sana leo kwetu. Hizo ndio mbinu za mpira lazima ufanye mambo kwa kuangalia utafaidika vipi, huko nyuma tumewahi kushinda michezo mingi dhidi ya waarabu tunapocheza saa 8:30 au saa 9:00.”

“Nasema hivyo kwa sababu hali ya hewa ya Cairo sasa hivi ni nyuzi joto kati ya 7 hadi 8 na kwa vyovyote vile itakavyokuwa, sisi watatuchezesha usiku ambapo hali ya hewa itakuwa ni nyuzi joto 7 ambayo itatu-affect kidogo kwa sababu kutakuwa na ubaridi ambao hatujauzoea labda Simba wende mapema zaidi.”

Mchezo wa leo ulipangwa kuchezwa saa 12:00 jioni ili kuwapa fursa mashabiki wengi kuhudhuria uwanjani kwa sababu mechi ilipangwa siku ya kazi (Jumatano, Februari 7, 2018).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here