Home Kitaifa “Kuna tatizo sehemu ya katikati”-mchezaji wa zamani Yanga

“Kuna tatizo sehemu ya katikati”-mchezaji wa zamani Yanga

7894
0
SHARE

Baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa raundi ya kwanza ya michuano ya vilabu bingwa Afrika kwa kukubali kipigo cha magoli 2-1, mchezaji wa zamani wa timu hiyo Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ ametoa maoni yake kwa kutaja eneo ambalo ameona lina mapungufu na huenda ndiyo sababu ya Yanga kupoteza mchezo.

Licha ya Yanga kupoteza mchezo wake wa nyumbani, bado Jembe Ulaya anaamini timu yake ya zamani bado ina nafasi ya kufuzu hatua ya makundi kwa kushinda mchezo wa ugenini dhidi ya Township Rollers endapo yatafanyika marekebisho.

“Mpaka hapa walipofika wamejitahidi, mechi hizi ni nyumbani na ugenini kinachotakiwa ni watu kutokata tama kwa sababu chochote kinaweza kutokea kama yatafanyika marekebisho kidogo.”

“Tatizo lililopo Yanga ni sehemu ya katikati ‘midifield’ pale kuna tatizo kubwa sana lakini nadhani kwa game kama hii ya leo mwalimu anaweza akafanya marekebisho game inayokuja lolote linaweza kutokea kwa sababu mpira wa siku hizi hauna nyumbani wala ugenini timu zinashinda popote, kwa hiyo hata kule Yanga wanaweza kupata matokeo.”

Endapo yanga wataondoshwa kwenye mashindano ya vilabu bingwa barani Afrika, wataangukia katika kombe la shirikisho Afrika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here