Home Kimataifa Kama Yanga wanahitaji kufuzu makundi waje Botswana na kitu kipya”-kocha Township

Kama Yanga wanahitaji kufuzu makundi waje Botswana na kitu kipya”-kocha Township

10417
0
SHARE

Kocha wa wa Township Rollers Nikola Kovazovic amesema, endapo yanga inahitaji kufuzu hatua ya makundi basi inahitaji kwenda na kitu kipya Gaborone, Botswana kwenye mechi yao ya marudiano ya klabu bingwa Afrika.

Kovazovic wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Yanga alisisitiza kuwa wakiendelea kubaki katika kiwango chao walichonacho sasa, Yanga inabidi wajipange.    

“Yanga ni klabu kubwa inahitaji kuheshimiwa lakini kama tutabaki katika kiwango hiki, watahitaji kuja na kitu kipya Gaborone kama wanataka kwenda hatua ya makundi”- Nikola Kovazovic.

“Tuanze kuangalia sisi tuliitoa klabu ya aina gani kwenye raundi ya awali, tuliwatoa El Merreikh ambao wanashika nafasi ya 50 kwa ubora katika vilabu vya Afrika, wao waliitoa timu kutoka Seychelles, na tukiangalia dakika 90 za mchezo wetu tulistahili ushindi zaidi ya tulioupata. Angalau tulipashwa kushinda kwa tofauti ya magoli matatu au manne.”

“Kabla ya huu mchezo niliingalia hii game mara 10 yaani nimewafutilia Rollers na Yanga mara 10 kabla ya kucheza leo hivyo nilikuwa na uwezo wa kutabiri kila kitu ambacho kingeweza kutokea.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here