Home Kimataifa Ni miaka 5 sasa Man City hajawai kupoteza nyumbani vs bingwa mtetezi,...

Ni miaka 5 sasa Man City hajawai kupoteza nyumbani vs bingwa mtetezi, leo vipi?

5754
0
SHARE

Kama Chelsea watashinda mchezo wao wa leo dhidi ya Manchester City baasi itakuwa mara yao ya kwanza kushinda michezo miwili mfululizo katika uwanja wa Manchester City tangu wafanye hivyo 2008.

Chelsea ndio wababe wa Manchester City katika EPL kwani City wamekubali kupoteza michezo 24 mbele ya Chelsea hadi sasa na Chelsea ndio timu inayoongoza kuwafunga Man City katika timu za EPL.

August 2015 ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa City kuifunga Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani, katika michezo yao minne ya mwisho nyumbani kwa City huo ndio ulikuwa mchezo wao pekee kushinda mbele ya Chelsea.

Tangu 2010 wapoteze kwa bao 1 kwa sifuri dhidi ya United, Manchester City hawajawahi kupoteza mchezo hata mmoja katika michezo yao mitano iliyofuata dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza.

Chelsea wanakwenda kuitembelea Manchester City katika kipindi kigumu sana kwani vijana wa Antonio Conte wamepoteza michezo yao mitatu iliyopita kati ya minne ikiwa ni michezo mingi kupoteza sawa na waliyopoteza mechi 23 zilizopita.

Manchester City wamepata ushindi katika michezo yao 13 iliyopita katika uwanja wa Etihad lakini katika michezo yao tisa ya mwisho katika uwanja huo ni michezo miwili tu ambayo City walifanikiwa kuwa na clean sheets.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here