Home Kimataifa Exclusive: Carlos Quieroz kuhusu Ronaldo, namna anavyoifahamu Tanzania na namna Iran walivyojipanga...

Exclusive: Carlos Quieroz kuhusu Ronaldo, namna anavyoifahamu Tanzania na namna Iran walivyojipanga na World Cup

11262
0
SHARE

Timu ya Taifa ya Iran inajiandaa kucheza mashindano ya kombe la dunia ifikapo June mwaka huu, baada ya kucheza katika michuano ya 2014 – na safari hii wapo kwenye mikono ya kocha Carlos Queiroz. Kocha huyo wa kireno nimekutana nae hapa Sochi – Russia, na yeye ni mmoja wa wahudhuriaji wa warsha ya FIFA World Cup 2018.

Nimefanya mazungumzo na Queiroz nilipokutana nae juzi kwenye Warsha na amezungumzia kwa kina matarajio yake kwa timu yake kwenye michuano hii.

Iran inakuja kwenye michuano hii tukiwa na mengi, kwa uzoefu tuliopata Brazil 2014 na huku wachezaji kadhaa wakipata nafasi ya kucheza barani ulaya – sasa tumeizidi kuimarika na kuwa washindani zaidi. Kucheza katika ya bara ya Asia sio sawa na kucheza soka katika anga ya Kimataifa. Hivi sasa tumekuwa bora. Iran ndio timu bora katika soka la bara la Asia kutokana na viwango vya FIFA, hatukupoteza mchezo hata mmoja katika kufuzu na tuliruhusu magoli machache. Hivyo tunaenda Russia tukiwa na matumaini ya kufanya vizuri kwenye kundi letu lenye timu za Spain, Ureno naMorocco

Nini malengo yenu: “Tunachotaka kwanza ni kuvuka hatua ya makundi, lakini hilo ni jambo gumu sana. Kila mmoja anakubaliana na ukweli kwamba kundi letu ni gumu sana kuliko lingine lolote kwa sababu tutakuwa tunaumana na timu mbili zinazopewa nafasi ya kutwaa ubingwa – Spain na Ureno. Lakini ni jukumu letu ni kwenda Russia na kupambana na kuhakikisha tunatimiza malengo, na hili litaendelea katika mashindano ya Asia na ngwe nyingine ya kufuzu kucheza World Cup 2022.”

Unajisikiaje kuhusu kukutana na timu ya Taifa unalotokea – Ureno?

Kama kocha wa Kireno nafikiri kucheza dhidi ya Ureno ni nafasi ya kipekee kwangu na wachezaji wangu. Itakuwa jambo la kuvutiaa kucheza dhidi yao na Spain pamoja na Morocco. Litakuwa lenye mechi za kuvutia sana katika kombe la dunia.”

Vipi kuhusu kukutana na Ronaldo mkiwa wapinzani uwanjani?

“Litakuwa jambo zuri na la kipekee, kama ambavyo inakuwa unapokutana na wachezaji wakubwa. Kwa hivi sasa, Ronaldo ni mchezaji bora wa dunia. Lakini mechi itakapoanza kutakuwa na timu mbili ambazo zote zinataka kushinda. Football itaamua nani ananshindasiku hiyo na nani atakuwa bora uwanjani siku hiyo.”

Unajisikiaje kuona wachezaji wa Iran wakiwa wanacheza soka katika ligi ya Russia – wachezaji kama Sardar Azmoun, Saeid Ezatolahi and Milad Mohammadi?

“Ni jambo muhimu sana. Ni sehemu ya maendeleo kwa wachezaji wa Iran. Mwaka 2011 tulikuwa na mchezaji mmoja tu aliyekuwa nchini Spain, lakini sasa asilimia 60 ya kikosi cha kwanza wanacheza barani ulaya, watatu kati ya hao wapo hapa Russia. Hili ni jambo muhimu kwa timu kwa sababu watatupa maarifa ya kuijua vizuri Russia na Warusi wenyewe. Hilo linaonyesha soka la Iran lilivyoendelea katika kila sekta.”

Mimi natokea Tanzania, Je unafahamu lolote kuhusiana na Tanzania?

“Yes nafahamu kuhusu Tanzania kwasababu nilizaliwa nchi ambayo karibu na Tanzania, nilizaliwa katika mji wa Nampula – Mozambique. Nimewahi kucheza dhidi ya Tanzania mwaka 1975, lakini pia wakati naifundisha South Africa 2002 nilicheza dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania. Wana wachezaji wazuri sana.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here