Home Kitaifa Yanga itavunja rekodi Mtwara?

Yanga itavunja rekodi Mtwara?

5974
0
SHARE

Leo Jumatano Februari 28, 2018 kutakuwa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ambapo Ndanda watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Nangwanda Sijaona kupambana na Yanga kuwania pointi tatu.

Yanga haina historia nzuri inapocheza na Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda-Mtwara. Mechi tatu ambao wamecheza katika uwanja huo hawajawahi kupata ushindi, wamepoteza mchezo mmoja na kutoka sare mara mbili.

 • Ndanda ?? Yanga
 • Yanga 1-0 Ndanda
 • Yanga 4-0 Ndanda
 • Ndanda 0-0 Yanga
 • Ndanda 2-2 Yanga
 • Yanga 1-0 Ndanda
 • Ndanda 1-0 Yanga
 • Yanga 0-0 Ndanda

Kwa sasa Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 18 pointi nane nyuma ya Simba ambayo inaongoza ligi baada ya kucheza mechi 19.

Yanga imeshinda mfululizo mechi zake tano za VPL za hivi karibuni, ndiyo timu pekee kwenye ligi ambayo imeshinda mechi nyingi katika mechi tano zilizopita. Simba imeshinda mechi nne na kutoka sare mchezo mmoja katika mechi tano zilizopita.

 • Ruvu Shooting 0-1 Yanga
 • Azam 1-2 Yanga
 • Lipuli 0-2 Yanga
 • Yanga 4-0 Njombe Mji
 • Yanga 4-1 Majimaji

Pamoja na kuwakosa wachezaji wengi kutokana na majeruhi, bado Yanga imeendelea kufanya vizuri kwa kutumia wachezaji wanaopata nafasi ya kuipigania timu yao.

Ndanda ina wachezaji wenye uzoefu wa ligi kama Jacob Masawe, Jabir Azizi Stima, William Lucian, Ame Ally, na kipenzi cha wana Yanga Mrisho Ngasa ambaye alicheza vizuri kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Ndanda haiko salama sana, imeshinda michezo mitatu tu msimu huu huku ikiwa imecheza mechi 18 bado wanapambana kuhakikisha wanasalia kwenye ligi kwa ajili ya msimu ujao.

 • Mbeya City 0-1 Ndanda
 • Ndanda 2-1 Lipuli
 • Stand United 0-1 Ndanda

Ndanda ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 18 (wastani wa kupata pointi moja kwa kila mechi iliyocheza).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here