Home Kimataifa Unajipanga kuja Russia kwenye World Cup? Hizi ndio gharama za tiketi, usafiri,...

Unajipanga kuja Russia kwenye World Cup? Hizi ndio gharama za tiketi, usafiri, malazi, vyakula na maisha kiujumla ndani ya Urusi

11031
0
SHARE

Huenda ukawa unatamani kuwa sehemu ya mamilioni ya wapenzi wa soka watakaofika nchini Russia kushuhudia michuano mikubwa zaidi ya soka duniani. Umebakia muda mfupi

sana kabla ya kuanza kwa mashindano haya.

Katika kukusaidia kufahamu gharama halisi na kupanga vizuri bajeti yako, nimefanya utafiti mdogo na kukuwekea taarifa za kina zitakazokusaidia kufahamu gharama utakazotumia kuweza kuwa sehemu ya historia ya kombe la dunia 2018.

1. Gharama za tiketi za mechi za FIFA World Cup.

Michuano ya FIFA World Cup Russia itafunguliwa mnamo June 14 itaendele mpaka July 15, 2018.

Baada ya kufungwa kwa mauzo ya tiketi ya awamu ya kwanza, jumla ya tiketi 742,760 zimeshauzwa. Hivyo sikushauri uendelee kusubiri zaidi – nunua tiketi yako sasa, usije ukakosa.

Bei za tiketi za sehemu ya katikati ya uwanja zinagharimu kuanzia kiasi cha $210 (takribani 450,000) kwenye mechi za makundi, mpaka kiasi cha $1,100 (2,250,000) kwa tiketi ya mchezo wa fainali.

Uwezo wa kuona mechi vizuri katika viwanja vya kisasa sio tatizo kabisa bila kujali utakaa wapi. Hivyo usijali unaweza kupunguza gharama kwa kuchukua tiketi za category 2 au category 3. Tiketi hizo zinagharimu kiasi cha $105 to $710 (laki 230,000 mpaka 1.5m). Pai kuna tiketi za category 4 – hizi ni tiketi maalum tu kwa Warusi; bei zake zinaanzia $20 mpaka $120.

2. Tiketi za Ndege

Usafiri pekee utakaoweza kukufikisha nchini Urusi ni usafiri wa anga, kwa uzoefu wangu kwenye safari yangu ya kutoka Dar es Salaam mpaka Moscow na kuja mpaka Sochi – tiketi ya ndege inagharimu mpaka kufikia kiasi cha $1,400 – takribani millioni 3 za madafu.

Bei hizi zitabadilika sana mpaka kufikia wakati wa kombe la dunia. Kutakuwa na uhitaji mkubwa wa usafiri wa ndege na hivyo bei zitapanda maradufu! Hivyo kama una mpango wa kuja huku fanya mipango ya usafiri mapema.

3. VizaBure

Kwa kawaida upatikanaji wa viza ya kuingia nchini Russia  ni mgumu sana kutokana na sheria za nchi hiyo hasa katika masuala ya usalama, hili kuondoa kasumba hii – wakatengeneza mfumo maalum ambayo utaondoa bugudha kwa wageni zaidi ya millioni na nusu ambao wanategemewa kusafiri kwenda Russia wakati wa kombe la dunia. Unapokuwa na FAN ID pekee utaweza kuingia katika mipaka ya nchi hii ya Russia bila kuhangaika kupata Visa. Hii ni moja ya faida kubwa ya kitambulisho hiki, hivyo unahitaji pasi ya kusafiria, tiketi yako na FAN ID ambayo mamlaka za Russia wanaitumia kama kadi ya kutambua wageni.

4. Malazi

Serikali ya Russia na timu ya maandalizi wamejitahidi sana katika suala la accommodation – kuna hotel, hostels na apartments za kutosha zilizoandaliwa kwa ajili ya mamilioni ya wapenda soka ambao watafika nchini humu wakati wa mashindano. Hata hivyo kuweza kumudu watu millioni 1.5 sio jambo jepesi na ndio maana watu wengi wameshaanza kufanya taratibu za malazi wakati wa World Cup! Hotels nyingi tayari zimeshajaa na hata zilizobako bei zimeanza kupanda maradufu hasa katika miji ya kitalii kama Moscow, St. Petersburg na Sochi. Kwa mfano hotel niliyofikia hapa mjini Sochi – Radisson Blu tayari imeshajaa yote kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao mashindano yatakuwa yanafanyika – FIFA wameichukua hotel kwa ajili ya wafanyakazi wao watakuwepo Sochi.

Serikali kupitia mamlaka za utalii wameanza kupambana na wenye hotels au Apartment ambazo zimepandisha bei kuliko kawaida – hivyo ukiachana na bei za ulanguzi ambazo zinafikia ongezeko mpaka la asilimia 18,000 – bei za kawaida kwenye hotel za nyota 5 zinaanzia $330 mpaka $700 kwa chumba cha hadhi ya kawaida.

Hotel ya nyota 3 inagharimu kiasi cha $100 mpaka $150.

Kuna baadhi ya maeneo wameandaa sehemu maalum za camping – kwa mfano katika mji wa Kaliningrand – kuna sehemu ya malazi ambayo ina unafuu kwenye bei – wanatumia tents ambazo zina uwezo wa kuchukua watu wawili kwa kila tent ambazo zipo katika uwanja mkubwa ambao upo mile 9 kutoka kwenye dimba litakalochezewa mechi za kombe la dunia. Kwa sasa tents hizo zipo kwenye mnada kupitia mtandao wa (booking.com) kwa ada ya $90.

5. Usafiri ndani ya Russia

Unaweza kupata usafiri wa bure ukiwa nchini Russia wakati wa Kombe la dunia, unachohitaji ni kuwa na tiketi za mechi pamoja na Kitambulisho kilichopewa jina la FAN ID – baada ya hapo utahitajika kujisajili kwenye mtandao wa tickets.transport2018.com – hapa utatengeneza akaunti na kuweza kufanya booking ya safari za ndani ya nchi hii kwa maana ya kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine miongoni mwa mikoa 11 ambayo michezo ya kombe la dunia itachezwa.

Kitu kingine unachotakiwa kufahamu umbali wa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ndani ya Russia ni mkubwa sana – safari ya treni inaweza kudumu mpaka kufikia saa 8, kama utahitaji usafiri wa haraka basi utahitaji kukwea pipa – bei ya tiketi kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine inaanzia $50 mpaka $350 kutegemeana na umbali wa sehemu husika.

Usafiri wa taxi haupo katika sehemu ya huduma za usafiri za bure, kwa mfano safari ya round trip katika mji wa Sochi inagharimu kiasi cha $7 mpaka $10, ila bado kuna wapigaji usipokuwa makini.

6. Vyakula na Vinywaji

Kwenye suala la vyakula na vinywaji kiukweli gharama sio kubwa sana! Na kuna kila aina ya vyakula kasoro vile vya kiswahili kabisa. Katika siku hizi 3 nilizokuwa hapa Sochi nimekuwa napata maakuli katika mgahawa wa Prince Wales – huu ni mgahawa wa kiingereza, hivyo kuna aina ya vyakula vyote vya asili ya bara ya ulaya, na bei ya mlo mmoja + maji au Juice, bei inaanzia kuanzia 40,000 mpaka 50,000 za kitanzania.

Lakini pia kuna restaurant tofauti tofuati kuanzia Chinese mpaka Indians ambazo wana mapishi ambayo kiasi yanaendana na mapishi ya nyumbani Tanzania kwa kiasi fulani – utapata mpaka chapati, wali, n.k ukiwa kwenye restaurants za kihindi.

:

Wenyeji hapa wanapendelea sana vyakula vya Sea Food – kuna upatikanaji mkubwa wa samaki aina mbalimbali ambao wanaotoka kwenye Black Sea!

Pombe huku ndio zinapotoka – bia zinauzwa kuanzia kiasi cha 10,000 mpaka 15,000 za kitanzania, Vodka inauzwa kuanzia $5 mpaka $10 kwa zile kawaida.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here