Home Kitaifa Historia imeandikwa Mtwara

Historia imeandikwa Mtwara

8189
0
SHARE

Kwa mara ya kwanza katika historia, Yanga imefanikiwa kupata ushindi kwenye ardhi ya Mtwara ikicheza dhidi ya Ndanda FC baada ya kuifunga 2-1 kwenye mchezo wa VPL uliochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kabla ya mchezo wa leo (Februari 28, 2018) timu hizo zilikuwa zinecheza mechi tatu kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Yanga haikuwahi kupata ushindi.

Ushindi huo wa Yanga dhidi ya Ndanda ni wa sita mfululizo kwenye ligi tangu iliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi sita zilizopita.

  • Ruvu Shooting 0-1 Yanga
  • Azam 1-2 Yanga
  • Lipuli 0-2 Yanga
  • Yanga 4-0 Njombe Mji
  • Yanga 4-1 Majimaji
  • Ndanda 1-2 Yanga

Yanga imefikisha pointi 40 ikiwa nyumba ya vinara wa ligi Simba yenye pointi 45 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 19.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here