Home Kitaifa Taarifa kutoka Simba kuhusu Okwi kuelekea mechi dhidi ya Stand United

Taarifa kutoka Simba kuhusu Okwi kuelekea mechi dhidi ya Stand United

14076
0
SHARE

Kama ulifuatilia mchezo kati ya ya Simba dhidi ya mbao uliochezwa Jumatatu Februari 26, 2018, utakuwa unafahamu kuwa Emanuel Okwi alitolewa uwanjani baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, taarifa kutoka Msimbazi zinaeleza kuwa, mchezaji huyo anaweza akashuka uwanjani kwenye mchezo ujao wa wa ligi Simba vs Stand United.

Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema, Okwi anaendelea vizuri na huenda akacheza kwenye mechi yao ya Ijumaa dhidi ya Stand United endapo kocha ataamua kumtumia.

“Okwi anaendelea vizuri aligongwa kidogo kwenye enka lakini anaendelea vizuri, kama mambo yatakuwa vizuri kesho atakuwa mazoezini. Wanachama wa Simba na mashabiki wasiwe na hofu, alipata jeraha dogo ambalo haliwezi kumsababishia akose mchezo unaokuja kama kocha ataamua kumtumia”-Haji Manara, afisa habari Simba.

“Timu inaingia kambini kesho kujiandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Stand United Ijumaa Machi 2, 2018.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here