Home Kimataifa Sio Messi wala CR7, Eden Hazard ni bora zaidi

Sio Messi wala CR7, Eden Hazard ni bora zaidi

10368
0
SHARE

Kampuni inayokusanya taarifa za takwimu mbali mbali za michezo iitwayo CIES Football Obsevatory imetoka na taarifa mpya kuhusu kiwango cha wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa kukokota mipira(dribles).

Takwimu zinaonesha barani Ulaya kwa sasa hakuna mchezaji yeyote anayemuweza mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard katika suala zima la kukokota mipira(dribles).

Inaonesha kwa asilimia 75 ya mipira ambayo Hazard alikokota ilifanikiwa kwenda anakoipeleka, Eden Hazard ana wastani wa 6.4 katika kila dakika 90 katika mipira aliyoikokota hadi sasa katika EPL.

Anayemfuatia Hazard ni mshambuliaji wa PSG Neymar ambaye ana dribbles nyingi katika dakika 90 akiwa amekokota mipira kwa wastani wa 7.4 lakini tatizo kwa Neymar ni kwamba katika wastani huo lakini amekamilisha 62% ya dribble zake.

Hii ni sawa na Lionel Messi ambaye 62% tu ya mipira aliyokokota ndio imefanikiwa, pamoja na ubora wote wa mchezaji huyu katika kukokota lakini msimu huu ana wastani wa 5.5 tu katika kila dakika 90.

Nafasi ya tano yuko Moussa Dembele wa Tottenham na Tanguy Ndombele wa Lyon, Cr7 hayuko katika 20 bora ya orodha hii lakini Paul Pogba wa Manchester United yupo katika nafasi ya 12.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here