Home Entertainment #Road2WorldCup – Sababu kwanini nipo Urusi kabla ya Kombe la Dunia kuanza

#Road2WorldCup – Sababu kwanini nipo Urusi kabla ya Kombe la Dunia kuanza

6018
0
SHARE

Ikiwa imebaki miezi mitatu na nusu kabla ya mashindano ya kombe la dunia 2018 kuanza nchini Russia, maandalizi ya mwisho yanaendelea katika nchi mwenyeji. Kwa timu shiriki 32 sasa ni wakati wa kufahamu zaidi kuhusu namna Russia walivyojipanga kuhusu mashindano haya.

Wiki hii, kuanzia leo tarehe 27 na kesho tarehe ya 28 ya mwezi February, kunafanyika Warsha maalum kwa ajili ya timu shiriki na waandishi wa habari katika mji wa Sochi.

Sochi – Huu ni mji uliopo katika jiji la Krasnodar Krai, Russia, uliopo karibu pwani ya Black Sea karibu na boda ya baina ya Georgia/Abkhazia na Russia.

Mji wenye wakazi wapatao 401,000, ulianzishwa mnamo mwaka 1838 na upo kilomita 1679 kutoka jijini Moscow.

Sochi ni moja ya mji mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia, mechi 6 za hatua ya makundi, mechi moja ya raundi ya 16 na mechi ya robo fainali moja – zitachezwa katika uwanja wa Fisht – uwanja ambao unaingiza mashabiki 48,000.

Team Workshop

Warsha hii ni muhimu na ni nafasi ya mwisho kwa nchi shiriki kufahamu kiundani maandalizi na mambo yote yanayohusiana mipangilio ya kombe la dunia. Kwa kuanzia leo kumekuwepo na maelekezo mbalimbali yanatoa majibu juu ya mambo kuhusiana na nchi mwenyeji, taratibu zake na mashindano kiujumla – kuanzia masuala ya usalama mpaka

Kwenye masuala ya ufundi.

Kati ya timu 32 zinazoshiriki World Cup 2018 – timu 5 tu ndio ambazo tayari zilishafika Russia mwaka mmoja uliopita katika Kombe la Mabara 2017: Germany, Portugal, Australia, Mexico na wenyeji Russia. Warsha hii ni nafasi ya mwisho kwa timu zote zinazoshiriki kukutana kabla ya kuanza kwa mashindano.

Nikiwa na kocha wa Iran – Carlos Quieroz

Wahudhuriaji ni akina nani?

Warsha hii imehusisha waandishi wa habari, makocha wa timu, madaktari, watu wa masuala ya ulinzi, watu wa masuala ya usafiri na masuala ya biashara na masoko.

Kiujumla warsha nzima ina ugeni wa watu 250, ambao wengi tuliwasili hapa Sochi siku ya Jumatatu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here