Home Kimataifa Road 2 World Cup: Bei za nyumba za kulala na hotel zapanda...

Road 2 World Cup: Bei za nyumba za kulala na hotel zapanda kwa asilimia 18,000 Russia

5756
0
SHARE

Katika moja ya vitu ambavyo nimegundua nikiwa hapa Sochi – Russia katika Warsha ya FIFA World Cup 2018 ni mambo mabadiliko makubwa ya bei za nyumba za kulala na hotels.

Hotel nyingi nchini Russia zimepandisha bei zao mpaka kufikia asilimia 18,000 wakitegemea kufanya biashara kubwa wakati wa mwezi 1 ambao mashindano ya kombe la dunia yatakuwa yakifanyika nchini humo.

Kwa mujibu wa utafiti mdogo niliofanya na timu yangu tukiwa hapa Russia – nyumba ya kulala wageni katika eneo la Kalinigrand – Apartment yenye vyumba 3 ina gharama ya £3,125 sawa na zaidi ya millioni 10 za kitanzania kwa usiku mmoja.

Kalinigrad ni mji ambao utahusisha mmoja ya mchezo mkubwa na ambao huenda ukaamua hatma ya timu mbili za England na Belgium ambao wamepangwa kundi A. Mchezo huo utafanyika 28 June na inaaminika kutokana na waingereza kufahamika kwamba watakuwepo wengi sana nchini Russia – basi wao ndio ni sehemu ya sababu za kupanda kwa bei za hotels na nyumba za kulala wageni.

Kwa kawaida Apartment ya vyumba vitatu katika eneo hili huwa haizidi £50, lakini sasa kumekuwa na ongezeko la asilimia 18,282

kupitia kampuni ya Airbnb, apartment ya chumba kimoja katika eneo hilo kwa sasa inapatikana kwa bei ya £1,000.

Sehemu pekee ya malazi ambayo ina unafuu kwa mashabiki ni tent ambazo zina uwezo wa kuchukua watu wawili kwa kila tent ambazo zipo katika uwanja mkubwa ambao upo mile 9 kutoka kwenye dimba litakalochezewa mechi za kombe la dunia. Kwa sasa tents hizo zipo kwenye mnada kupitia mtandao wa (booking.com) kwa ada ya £63 kwa siku hiyo ya mchezo wa England vs Belgium. Eneo hilo limepewa jina la “Camping for Tents” – lipo katika kijiji cha Petrovo, Kaskazini Magharibi mwa mji wa Kaliningrad.

.

Michuano ya World Cup inafunguliwa rasmi jijini Moscow mnamo tarehe 14 wakati wenyeji Russia watakapocheza dhidi ya Saudia Arabia, na yatafungwa katika fainali itakayochezaa 15 July. Kumekuwepo na mabadiliko ya sheria katika upatikanaji wa Visa ya kuingia Russia kuanzia sasa ili kuweza kusaidia mashabiki wenye tiketi au kadi za ushabimi kupata vida kiurahisi – Visa ambayo inakupa fursa ya kutumia mabasi na treni za safari za ndani bure.

Baada ya kuondolewa kwa masharti magumu katika kupata visa ya kuingia Russia, sasa inategemewa watu wengi kutoka kila pembe ya dunia watakuja hapa kushuhudia kombe la dunia – hasa mashabiki kutoka nchi za England, France, Ujerumani na Poland. Mamlaka za Russia zinatabiri watapokea wageni angalau millioni na nusu kwa ajili ya kombe la dunia na sasa wamejipanga kuanza kuweka mazingira sawa ya watu hapa kudanguliwa na wafanyabiashara.

Mamlaka za utalii za Russia kupitia wachunguzi wake zimekuwa zikitaja na kuchukulia hatua baadhi ya hotels ambazo zimekuwa zikipandisha kubwa pasivyo halali. Moja ya hotel kubwa ambayo inatuhumiwa kudangua bei ni Agora Hotel, ambayo ipo karibu na uwanja wa Kaliningrad – ipo juu kwenye listi ya hotels 50 ambazo zimetuhumkwa kupandisha bei isivyo halali.

Kitengo cha Utalii cha Russia (Rosturizm) kimezitaja pia Tikhiye Sady (“Quiet Garden”), hotel ambayo ipo jijini Rostov-on-Don, kwa kuongeza bei kwa asilimia 25 wakati wa siku utakapochezwa mchezo wa Brazil vs Switzerland mnamo tarehe 17.

Jijini Moscow, Hotel Petrovka 17 — inatuhumiwa kuongeza zaidi ya mara 4 ya bei ya kawaida mpaka kufikia kiasi cha £440 (takribani millioni 1.5 za kibongo) kwa siku wakati wa kipindi cha kombe la dunia.

Mji huo mkuu wa Urusi una viwanja viwili ambavyo vitatumika kwa ajili ya michezo ya kombe dunia: Luzhniki ambao utatumika kwa ajili ya ufunguzi na fainali, na uwanja wa Spartak. Mji huu ndio ambao waandishi wa habari wengi na wageni wengi watafikia Na hivyo ulanguzi mkubwa unafanyika ndani ya Moscow.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here