Home Kimataifa Rashidi Mandawa ameisafishia njia Yanga Botswana

Rashidi Mandawa ameisafishia njia Yanga Botswana

11854
0
SHARE

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka tanzania anaecheza soka kwenye klabu ya BDF XI Rashid Mandawa, jana Jumatatu Februari 26, 2018 amefunga hat-trick dhidi ya township rollers ambao ni wapinzani wa yanga kwenye mchezo unaofuata wa hatua ya kwanza ya michuano ya vilabu bingwa Afrika (Caf Champions League).

Mandawa alifunga magoli hayo matatu kwenye mchezo wa ligi na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 ambao umeifanya ifikishe pointi 29 baada ya kucheza mechi 19 huku ikiwa kwenye nafasi ya sita ya msimamo wa ligi.

Hat-trick aliyofunga Mandawa dhidi ya Township Rollers imemfanya afikishe magoli 11 kwenye ligi kuu ya Botswana (BWPL) huku akiwa ametoa assists tano.

“Tangu nimejiunga na bdf nimefunga magoli nane na pasi tano za magoli (kabla ya mchezo dhidi ya township rollers)”-Mandawa.

Mandawa ameielezea kwa kifupi klabu ya Township Rollers ambayo kama wangekubabaliana huenda angekuwa anaitumikia kwa sababu kabla ya kujiunga na BDF alifanya majaribio kwenye klabu hiyo lakini hawakufikia makubaliano ili aweze kucheza kwenye timu hiyo.

“Kwa hapa Botswana Township Rollers ni timu kubwa kwa sababu ipo ki-professional zaidi, ukichagua timu bora inayoweza kushiriki ligi ya South Africa, Township rollers inaweza kuwa timu ya kwanza kwa sababu ina kila kitu, kwa Tanzania tunaweza kuifananisha na Azam kwa sababu Azam wana uwanja wao na kila kitu.”

“Ni timu kubwa yenye mashabiki wengi kama Yanga ilivyo tanzania. Township Rollers inashabikiwa karibu sehemu zote za Botswana na miongoni mwa timu inayopendwa sana. Yanga wanatakiwa kujua wanakutana na timu kubwa.”

“Safu yao ya ushambuliaji ndio hatari sana, wanaweza kuamua matokeo wakati wowote.”

Alivyopata mchongo kusukuma ngozi nje ya nchi

“Kuna mtu alinipa connection, sikuanzia hapa BDF XI nilianzia Township Rollers nikafanya trials pale lakini hatukukubaliana kwa hiyo nikahamia BDF  ambako nipo hadi sasa naendelea kufanya kazi

Ttofauti ya soka la Botswana na nyumbani

“Maisha ya Botswana kwa upande wa soka ni yaleyale na mara nyingi maisha ya mpira huwa hayabadiliki sana zaidi ni kupambana tu hakuna kinachobadilika.”

Samatta anampa machungu yasiyopimika

Maisha ya mpira ni mafupi sana, lakini ndoto zangu ni kufika mbali sana sio kucheza tanzania tu, nataka kufika mbali zaidi ili kuwa mfano bora zaidi kama anavyofanya mtanzania mwenzetu Mbwana Samatta kwa hiyo nataka kufika huko au zaidi ya alipo Samatta. Nasikia uchungu nikifikiria mwenzetu amefika vipi huko na sisi tunashindwa vipi.

Uendeshaji wa soka Botswana

Utofauti sio mkubwa sana mambo ni yaleyale lakini huku wenzetu wapo ki-professional zaidi kwenye level ambayo tunaweza kuifikia lakini tutachelewa. Ligi yao ni ngumu sana, ligi ya hapa na South Africa hazijapishana sana, kutoka botswana kwenda South Africa sio mbali sana na sio kazi kubwa kama unaonesha kiwango basi kwenda South Africa inkuwa kazi rahisi kuliko kutoka Tanzania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here