Home Kimataifa Herrera kwenda jela miaka 4 na kufungiwa soka miaka 6

Herrera kwenda jela miaka 4 na kufungiwa soka miaka 6

24317
0
SHARE

Kulikuwa na kesi ambayo ilikuwa ikiihusisha klabu ya zamani ya kiungo wa Manchester United Zaragoza ambapo May mwaka 2011 walihusishwa na kupanga matokeo pamoja na klabu ya Levante.

Kesi kuhusu tukio hilo ilikuwa bado inaendelea nchini Hispania lakini sasa mawakili wanaosimamia kesi hiyo wameibuka na kuitaka mahakama kutoa hukumu ya miaka 4 jela kwa wahusika wa kesi hiyo.

Mara nyingi kesi za watu maarufu nchini Hispania huwa chini ya miaka 2 hali inayowapelekea kutumikia kifungo nje ya gereza lakini sasa kwa Ander Herrera upande wa washtaki umependekeza kutolewe adhabu ya miaka 4 gerezani.

Sio tu kwenda jela miaka 4 lakini pia mahakama imetakiwa kutoa adhabu ya kutojihusisha soka kwa miaka 6 baada ya kutoka jela kwa Herrera pamona na wenzake 35 ambao walihusika katika tukio hilo.

Ushindi wa Zaragoza wa mabao 2 kwa 1 vs Levante mwaka 2011 uliwafanya Derpotivo La Coruna kushuka daraja matokeo ambayo baadae iligundulika kwamba Levante na Zaragoza walipanga matokeo.

Pia Herrera na wenzake wanatakiwa kutoa faini £2.9m kila mmoja, wachezaji wengine katika kesi hii ni pamoja na Gabi wa Atletico Madrid, wengine ni Christian Stuani wa Middlesbrough, bado La Liga hawajatoa maoni yao kuhusu kesi hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here