Home Kitaifa Yanga yalia na ratiba VPL, FA, CAF

Yanga yalia na ratiba VPL, FA, CAF

10325
0
SHARE

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia msemaji wake Dismas Ten asema klabu yao inakabiliwa na ratiba ngumu ya mshindano mbalimbali wanayoshiriki msimu huu.

Februari 21, 2018 Yanga imecheza mechi yake ya Caf Champions League dhidi St. Louis nchini Seychelles, Jumapili ya Februari 25, 2018 itacheza FA Cup dhidi ya Majimaji mjini Songea na Jumatano Februari 28, 2018 itatakiwa kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara mkoani Mtwara dhidi ya Ndanda

“Ratiba imebana kidogo lakini hakuna namna ndivyo ratiba ilivyo tuna mashindano ya kimataifa pia kwa sababu baada ya mchezo wa Mtwara tutakwenda kucheza Morogoro baadae tutarudi Dar Machi 6, 2018 kucheza na Township Rollers mchezo wa klabu bingwa”-Dismas Ten.

“Fifa imeagiza kwamba mashindano yote yanatakiwa kumalizika mwezi Mei kwa hiyo ratiba imewekwa hivyo, inatuwia vigumu lakini wakati mwingine tunalazimika kusema malalamiko yetu kuhusiana na ratiba lakini mwisho wa siku inabidi tucheze, kwa sababu inabidi ucheze kwanza halafu upeleke malalamiko mengine baadaye.”

Baada ya mchezo wa Mtwara dhidi ya Ndanda, Yanga itakwenda kucheza Morogoro dhidi ya Mtibwa sugar kisha itarejea Dar kusubiri mechi yao ya kimataifa machi 6, 2018 dhidi ya Township Rollers.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here