Home Kimataifa “Tunahitaji ushindi kuliko kitu chochote”Cannavaro

“Tunahitaji ushindi kuliko kitu chochote”Cannavaro

5523
0
SHARE

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema hakuna kingine ambacho wanahitaji zaidi ya ushindi kwenye mchezo wao Caf Champions League ikiwa ni mechi ya marudiano ugenini dhidi ya St. Louis ya Seychelles.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu sana, tumejipanga vizuri na yeyote atakaepata nafasi atacheza kwa asilimia 100 ili kuisaidia timu kwa sababu mchezo wa leo tunahitaji kupata matokeo mazuri”-Cannavaro

“Tunajua kwamba tunacheza na timu nzuri lakini kwa upande wetu hakuna kitu kingine tunachohitaji zaidi ya ushindi kwa sababu huku tumekuja kuwakilisha nchi.”

“Tunaongoza kwa goli 1-0, sio dogo lakini tunahitaji kulilinda ili tusiruhusu goli.”

Yanga ilishinda goli 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here