Home Kitaifa “Tumekuja na style ya kuwapapasa”-Masau Bwire

“Tumekuja na style ya kuwapapasa”-Masau Bwire

6451
0
SHARE

Baada ya Ruvu Shooting kupata ushindi wa ugenini wa magoli 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu Complex, afisahabari w Ruvu Shooting amesema hiyo ni style yao mpya kwa sasa inayojulikana kama ‘papasa’.

Timu hizo zilikuwa zinacheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, Mtibwa ndio walianza kupata bao kupitia kwa Ismail Mhesa lakini baraka Mtuwi aliisawazishia Ruvu kabla ya Issa Kanduru kufunga bao la ushindi.

Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire ameelezea kuhusj style yao mpya ya kupapasa.

“Tulisema kila atakaepita mbele yetu lazima tumpapase na ndio tunachokifanya, tulitamka kabla tunakwenda kuwapapasa Mtibwa baada ya kuwapapasa kadhaa waliopita”-Masu Bwire afisa habari Ruvu Shooting.

“Tulipokelewa vizuri na Thobias Kifaru na nikamweleza kwamba tumekuja kwa dhamira moja ya kuwapapasa Mtibwa, hakuelewa alishtuka kidogo nikamwambia tutakupapasa utazoea na ndicho kilichotokea.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here