Home Kimataifa Messi ataonea wengine lakini kwa Chelsea ni nyoka wa kibisa tu

Messi ataonea wengine lakini kwa Chelsea ni nyoka wa kibisa tu

5890
0
SHARE

Lionel Messi ni kati ya wanasoka ambao ukitaja wanasoka watatu kuwahi kutokea duniani baasi jina lake lipo na kwa wengi hata ukitaka kutaja jina la mchezaji mmoja baasi utakuta jina la Lionel Messi ndio linatajwa.

Messi anatisha na Messi anaogopesha, lakini cha ajabu na kustaajabisha ni kwamba Messi anaogopwa na kuonea watu wengine lakini akifika mbele ya Chelsea anakuwa nyoka wa kibisa (hana sumu).

Toka aanze kucheza soka la kimataifa katika klabu ya Barcelona hadi hivi sasa Lionel Messi amefunga jumla ya mabao 595 na ni mabao 5 tu kufika 600 lakini hadi hivi sasa hajawahi kugusa wavu wa Chelsea hata mara moja.

Chelsea ndio wanashikilia rekodi mbovu ya Messi kwani tangu aanze kupiga soka hajawahi kukutana na timu mara nyingi halafu asifunge kama ilivyo Chelsea, wameshakutana mara nane.

Msimu wa mwaka 2005/2006 katika hatua kama hii Barca waliwatoa Chelsea kwa jumla ya mabao 3 kwa 2 na Messi hakufunga, 2006/2007 Chelsea wakalipiza kwa Barcelona na kuwaondoa kwa bao la Didier Drogba nayo pia Messi hakufunga.

2008/2009 Messi alikuwepo kikosi cha Barca kilichokwenda fainali na hakuifunga Chelsea japokuwa yeye ndio alikuwa mpishi wa bao la Andres Iniesta lilioiondoa Chelsea katika michuano hiyo.

2011/2012 tena ikiwa mara ya 4 kukutana katika Champions League(sawa na mechi 8) Messi alishuhudia Barcelona wakiondolewa katika Champions League na akikamilisha idadi ya mashuti 29 langoni mwa Chelsea bila bao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here