Home Kimataifa Mechi yaahirishwa baada ya kadi nyekundu 9 kutolewa nchini Brazil

Mechi yaahirishwa baada ya kadi nyekundu 9 kutolewa nchini Brazil

9923
0
SHARE

Hii imetokea nchini Brazil baada ya mchezo kati ya Vitoria na Bahia baada ya wachezaji sita kutoka katika timu wenyeji ya Vitoria kupewa kadi nyekundu katika mchezo huo na mchezo ukiwa na jumla ya kadi nyekundu tisa.

Mchezo huo wa Derby kati ya timu hizo ulipigwa siku ya jana lakini zikiwa zimebaki dakika 11 kwa mchezo huo kuisha kulitokea fujo uwanjani zilizomfanya muamuzi kugawa kadi nyekundu kama njugu.

Fujo kubwa ilianza baada ya Bahia kusawazisha bao la kuongoza la Vitoria ndipo mchezaji wa Bahia akaenda kushangilia kwa ishara ya kucheza ambayo haikuwa nzuri mbele ya mashabiki wa Vitoria.

Hii iliamsha hasira kwa wachezaji na mashabiki wa Vitoria na ndipo ngumi zikaanza kupigwa na wachezaji watatu kutoka Vitoria na wawili kutoka Bahia walipewa kadi nyekundu wakati wa mvutano huo.

Dakika chache baada ya fujo hizo mpira ulisimama tena na safari hii pia ilikuwa ni kutokuelewana kati ya wachezaji wawili wa timu hizo na wote wakala kadi nyekundu.

Zikiwa zimebaki dakika 13 kwa mchezo kuisha mchezaji wa Vitoria mwingine alipewa kadi nyekundu kabla ya mfungaji wa bao la kwanza la wenyeji kupewa kadi ya pili ya njano baada ya kujibizana na muamuzi.

Hadi dakika 11 kabla ya mchezo huo kuisha ilishuhudiwa Vitoria wakibaki na wachezaji 5 uwanjani hali iliyopelekea muamuzi kuahirisha pambano hilo kwani sheria zinakataza timu kuwa na wachezaji chini ya saba uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here