Home Kimataifa Sababu kubwa iliyomkimbiza Pogba kutoka United 2012 yabainika

Sababu kubwa iliyomkimbiza Pogba kutoka United 2012 yabainika

8057
0
SHARE

Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes amefunguka kuhusu sababu iliyompelekea kiungo wa Manchester United Paul Pogba kuikimbia klabu hiyo mwaka 1992.

Katika mahojiano yake na moja ya kituo cha habari barani Ulaya, Scholes amesema kati ya vitu ambavyo vilimfanya Pogba kufunga virago na kuamua kuondoka zake alikuwa Phill Jones.

Siku huyo ilikuwa katika mchezo kati ya Manchester United na Blackburn Rovers ndipo kocha SAF aliamua kumpa nafasi Phill Jones katik kikosi cha kwanza na kumtosa Pogba.

Inadaiwa kwamba jambo hilo lilimkera sana Pogba kwani alikuwa anajua kwamba Jones ni mlinzi wa kati hivyo inakuaje kwake kupewa namba kikosi cha kwanza tena katika kiungo huku yeye akitosa.

Scholes anasema kwamba kikosi cha United kilikuwa na majeruhi wengi na Pogba alitaraji Alex Fergson anaweza kumpa nafasi siku hiyo lakini alitoswa 

Scholes ambaye anasema aliahidiwa nafasi ya ukocha wa reserve anasema lilikuwa suala sahihi kwa Pogba kukimbia kwani Fergie hakuwa anaonekana kuwa na mpango naye.

Pogba aliondoka na kukimbilia Italia alipojiunga na klabu ya Juventus na baadae akafanikiwa kuwa kati ya wachezaji wakubwa duniani kiasi cha kuwapeleka United kumrudisha kwa ada ya rekodi ya dunia £89m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here