Home Kitaifa “Bocco atasafiri hata kama hatocheza”-Simba

“Bocco atasafiri hata kama hatocheza”-Simba

9852
0
SHARE

Nahodha wa Simba John Bocco anatarajia kusafiri na timu kwenda Djibouti kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Caf Champions League dhidi ya Gendarmerie ingawa hakuna uhakika kama mshambuliaji huyo atacheza katika mchezo huo.

Bocco aliumia kifundo cha mguu wa kushoto wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui uliochezwa Alhamisi Februari 17, 2018 kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga na kushindwa kuendelea na mchezo.

Mjumbe wa kamati ya utendaji Simba, Said Tully amesema Bocco atasafiri na timu lakini walimu wamepanga kumpumzisha katika mchezo huo wa kimataifa.

“Bahati nzuri John Bocco hali yake sio mbaya ingawa walimu wanatarajia kumpumzisha kwenye mechi yetu tunayoenda kucheza Djibouti lakini ataambana na timu kwa sababu yeye ni captain, pamoja na kucheza ana jukumu la kuhamasisha wenzake ili kuweza kupata ushindi na kuendelea katika raundi ijayo”-Said Tully ameiambia Radio One.

Kikosi cha Simba kinatarajia kusafiri Jumamosi Februari 18, 2018 kuelekea Djibouti na wanatarajia kucheza siku ya Jumanne Februari 20, 2018. Mchezo wa kwanza Simba ilishinda 4-0 dhidi ya Gendarmeie kwenye uwanja wa Taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here