Home Kimataifa Rodger Federer ampiga kikumbo Rafael Nadal na kuwa “mhenga namba moja” katika...

Rodger Federer ampiga kikumbo Rafael Nadal na kuwa “mhenga namba moja” katika tennis

4414
0
SHARE

Rodger Federer anaonekana kuendelea kutakata pamoja na umri kumtupa mkono kwani siku chache baada ya kutoka kupata Grand Slam yake yake ya 20, sasa anakuwa mchezaji namba moja katika mchezo wa tennis duniani.

Sio tu kukwea hadi nafasi ya kwanza bali pia Federer sasa anakuwa mchezaji wa kwanza kushika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya tennis ulimwenguni huku akiwa na umri mkubwa (36).

Federer anashika usukani wa viwango vya tennis baada ya miaka mitano kupita na hii inakuja baada ya kumchapa Robin Haase katika robo fainali ya dunia ya tennis.

Federer alishinda mchezo huo kwa jumla ya seti 4-6,6-1 na 6-1 sasa anakaa juu ya mpinzani wake mkubwa ambaye ni Rafael Nadal katika viwango hivyo kwa mujibu wa ATP.

Kabla ya Federer kuweka rekodi hii ya kuwa mcheza tennis namba moja mwenye umri mrefu, rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na Andre Agassi ambaye yeye aliwahi kuwa namba moja kwenye viwango vya tennis akiwa na miaka 33.

Pamoja na rekodi yake kuvunjwa lakini Agassi alikuwa mtu wa kwanza kumpongeza Federer kupitia Twitter huku akimtakia mafanikio makubwa zaidi na rekodi kubwa nyingine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here