Home Kitaifa Daktari Simba kazungumzia majeraha ya Bocco

Daktari Simba kazungumzia majeraha ya Bocco

15728
0
SHARE

Daktari wa Simba Yassin Gembe ametoa ufafanuzi kuhusu majeraha ambayo amepata John Bocco kwenye mchezo wa Mwadui vs Simba.

Bocco aliumia dakika chache kabla kipindi cha kwanza kumalizika, aliumizwa na Revocatus mlinzi wa Mwadui.

“Ameumia kifundo cha mguu wa kushoto anahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini kwa uchunguzi wa awali tuliomfanyia inaonekana ni jeraha la kawaida na hatokuwa nje kwa muda mrefu”-Yassin Gembe.

Kabla hajaumia Bocco aliifungia Simba bao la kwanza mapema dakika ya 10 kipindi cha kwanza, baada ya kushindwa kuendelea na mchezo Laudit Mavugo aliingia kuchukua nafasi yake.

Goli alilofunga jana Bocco dhidi ya Mwadui limemfanya afikishe magoli 10 kwenye ligi akiwa na Simba msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here